Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga amabaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya lishe Wilayani humo Bw. Tano John Malele akizungumza Julai 16, 2025 katika kikao maalum cha kujadili Taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha robo ya nne (Aprili - Juni) mwaka wa fedha 2024/2025, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo
Na Sumai Salum, Kishapu
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe ya Wilaya hiyo Bw. Tano John Malele, amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kuongeza umakini katika kusimamia masuala ya lishe hasa katika Shule za Msingi na Sekondari, ili kuimarisha afya na ufaulu wa wanafunzi.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Joseph Swalala akizungumza Julai 16, 2025 katika kikao maalum cha kujadili taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha robo ya nne (Aprili - Juni) mwaka wa fedha 2024/2025, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo
Afisa lishe Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Hadija Nchakwi akizungumza Julai 16, 2025 katika kikao maalum cha kujadili taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha robo ya nne (Aprili - Juni) mwaka wa fedha 2024/2025, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo

Akizungumza Julai 16, 2025 katika kikao maalum cha kujadili Taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha robo ya nne (Aprili - Juni) mwaka wa fedha 2024/2025, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Malele amesisitiza umuhimu wa lishe katika kupunguza utoro na kuongeza ufaulu mashuleni.
“Ndugu zangu Watendaji, suala la lishe si la pembeni. Serikali ya awamu ya sita imetoa kipaumbele kwa watoto kupata chakula mashuleni. Robo ijayo hatutaki kusikia shule yoyote haina uji wala chakula cha mchana kwa wanafunzi wa Sekondari,” amesema Malele kwa msisitizo.
Amewakumbusha Watendaji kuwa Kiongozi na kielelezo hivyo wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kujitolea katika kuhamasisha jamii kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi, akiwataka pia wasimamizi wa vyakula hivyo kuwa waaminifu katika usimamizi wake.
Katika kikao hicho, Mtendaji wa Kata ya Mwamashele ametunukiwa zawadi ya fedha taslimu kwa kutekeleza vyema majukumu ya lishe, sambamba na mwandishi mmoja wa vikao vya halmashauri na mtumishi kutoka shirika la WordVision.
Kwa upande wake, Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala amewataka watendaji waendelee kutoa elimu ya lishe bora kwa jamii huku wakihamasisha ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa afua hizo.
Afisa Lishe wa Wilaya hiyo, Bi. Hadija Ahmed Nchakwi, ameipongeza serikali kwa juhudi kubwa za kupambana na udumavu kwa watoto wenye umri wa miezi 0 hadi 59 pamoja na wajawazito akisema kiwango cha udumavu kimeanza kushuka kutokana na ongezeko la uelewa kwa jamii, licha ya kuwepo changamoto kama upungufu wa chakula mashuleni na kutotekelezwa kwa maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ngazi ya vijiji.
“Jamii inaanza kuachana na mazoea ya kula bila mpangilio hata wajawazito wanapokuja kliniki pamoja na watoto wao tunaona dalili za wazi za kupungua kwa udumavu,” amesema Nchakwi.
Kwa mujibu wa takwimu, Wilaya ya Kishapu ina jumla ya shule 168 za msingi na sekondari. Katika robo ya tatu, shule 152 sawa na asilimia 90.5% zilikuwa zikitoa chakula kwa wanafunzi, huku robo ya nne idadi hiyo ikiongezeka na kufikia asilimia 97.62%.
Taarifa tisa (9) zimewasilishwa katika kikao hicho, kutoka idara mbalimbali zikiwemo Idara ya Afya,Ustawi wa Jamii na lishe, Elimu ya Awali na Msingi,Elimu Sekondari, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Maendeleo ya Jamii, Ruwasa, Redeso pamoja na viongozi wa dini kutoka madhehebu ya Kiislamu.
Kikao hicho kimeonesha kuwa mafanikio katika vita dhidi ya udumavu,kushuka kwa ufaulu na utoro mashuleni yanahitaji ushirikiano wa pamoja kati ya viongozi, jamii na wadau wa maendeleo huku kipaumbele kikubwa ni kuwekeza katika lishe bora kama msingi imara wa elimu bora kwa watoto wa Kishapu.

Social Plugin