Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UJUMBE MAALUM: SIKU YA BABA DUNIANI –MALUNDE BLOG INAWAENZI MASHUJAA WA FAMILIA



Leo dunia nzima inaadhimisha Siku ya Baba Duniani ,siku maalum ya kutafakari, kuenzi na kusherehekea mchango wa Baba katika maisha ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Katika maisha ya kila siku, Baba ni zaidi ya mlezi.
Ni nguzo, ni kiongozi wa familia, ni mlinzi wa ndoto za watoto wake na ni mfano wa maadili kwa vizazi vijavyo.

Mchango wake mara nyingi huonekana kimya kimya kupitia jasho analotoka kazini, maamuzi ya busara anayofanya kwa ajili ya ustawi wa familia, au hata kwa ushauri unaobeba hekima isiyo na mwisho.

Katika nyakati za changamoto, Baba ndiye anayebeba mzigo kwa kifua kipana hubeba maumivu.

Katika nyakati za furaha, yeye hupiga hatua nyuma ili watoto wake wapendeze na kufurahia maisha. Ni sauti ya utulivu katikati ya dhoruba, na ni nguvu ya kutusukuma kusonga mbele hata tunapohisi kuchoka.

Leo tunatambua na kumthamini kila Baba aliye mzazi wa damu,aliye mlezi kwa mapenzi, au hata Baba wa kiroho na mfano bora wa uongozi wa kiume.

Tunawaenzi Baba waliopo nasi, na tunawakumbuka kwa heshima wale waliotutangulia mbele ya haki.

Tunawatambua wale wanaojitahidi kuwa bora kila siku, licha ya changamoto nyingi wanazopitia katika dunia inayobadilika kwa kasi.

Katika siku hii muhimu, tujikumbushe kutamka maneno rahisi lakini yenye nguvu: "Asante Baba."

Asante kwa upendo usio na masharti, kwa kujitoa bila kuchoka, na kwa kutufundisha thamani ya juhudi, heshima na ujasiri.

Kwa niaba ya familia yetu ya wasomaji wote wa Malunde 1 Blog tunawatakia Baba wote duniani Siku Njema ya Baba iliyojaa furaha, heshima na baraka tele.

Imeandaliwa na Dotto Kwilasa_0786434347

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com