Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAKUSUDIA KUKUSANYA TRILIONI 34.10 KUPITIA TRA 2025/26


Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba

Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kukusanya jumla ya Shilingi trilioni 34.10 katika mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwa ni mapato ya kodi na yasiyo ya kodi.

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 4, 2025, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha.

Dkt. Nchemba ameeleza kuwa kati ya kiasi hicho, Shilingi trilioni 32.31 zinatarajiwa kutokana na mapato ya kodi, huku trilioni 1.79 zikitarajiwa kutoka kwenye vyanzo visivyo vya kodi.

Ameongeza kuwa TRA itaendelea kuboresha mifumo ya usimamizi wa mapato kwa njia ya kielektroniki kama vile TANCIS na IDRAS, sambamba na kuimarisha utoaji wa elimu ya kodi kwa umma.

“Kupitia maboresho haya, tunalenga kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato, kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari, na kupunguza mianya ya upotevu wa mapato inayotokana na udanganyifu wa taarifa za miamala na biashara za magendo,” amesema Waziri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com