Diwani wa kata ya Bwilingu Nasser Karama akiagana na Mch. Joseph Hananja. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw. Shaibu Ndemanga
NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Shaibu Ndemanga, ameyapongeza makanisa yanayounda Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa ajili kongamano la kuliombea Taifa, leo katika viwanja vya polisi katika halmashauri ya Chalinze,Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Kongamano hilo limeandaliwa na CCT kupitia matawi yake ya Chalinze na limehudhuriwa na waumini kutoka zaidi ya makanisa kumi yanayounda jumuiya hiyo.
Dhumuni la kongamano hilo ni kuliombea Taifa la Tanzania na kuhimiza amani na mshikamano nchini.
" Ninawapongeza viongozi wa CCT mkiongozwa na Mwenyekiti wenu, Mchungaji Joseph Chuma wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kwa kuonyesha maono makubwa ya kiroho na uzalendo kwa taifa letu", amesema mkuu wa Wilaya.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisisitiza mshikamano kwa waumini na kuwataka wawe mabalozi wa amani bila kusahau malezi kwa vijana wetu dhidi ya madawa ya kulevya.

Kongamano hilo, lilihudhuriwa pia na Mchungaji Richard Hananja, ambapo aliwahimiza waumini kuendelea kusimama katika nafasi yao ya maombezi kwa ajili ya Taifa huku akisisitiza kuwa kanisa lina jukumu kubwa la kuiongoza jamii kiroho na kijamii.
Social Plugin