Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HAILU HEMED MUSSA AONYESHA NIA YA KUENDELEA KUHUDUMIA WANANCHI KATA YA MCHANGANI



Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru na Diwani wa Kata ya Mchangani akikabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya udiwani katika kata ya Mchangani wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma 

Na Regina Ndumbaro Tunduru-Ruvuma 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru na Diwani wa Kata ya Mchangani, Ndugu Hailu Hemed Mussa, ameibuka tena kwa kishindo baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya udiwani kwa mara nyingine katika kata hiyo, akionesha dhamira ya kuendeleza kazi ya kuwatumikia wananchi. 

Hatua hiyo imepokelewa kwa hamasa kubwa na wakazi wa Mchangani waliompongeza kwa moyo wa kujitolea aliouonesha katika vipindi vya nyuma.

Ndugu Hailu, ambaye anasifika kwa kusimamia miradi ya maendeleo na utatuzi wa changamoto mbalimbali za wananchi wakati wa uongozi wake, amesema anaamini bado ana mengi ya kuwatumikia wakazi wa Mchangani kwa ufanisi zaidi ikiwa atapewa ridhaa ya kuendelea na nafasi hiyo. 

Ameeleza kuwa azma yake ni kuendeleza kazi aliyoianza kwa kuzingatia ilani ya Chama cha Mapinduzi na maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Hailu amewahakikishia wananchi kuwa ataendelea kuwa kiongozi wa karibu kwao, anayesikiliza na kutatua kero kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka husika. 

Aidha, amesisitiza kuwa ataimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kasi na kwa viwango vinavyotakiwa.

Wananchi wa kata ya Mchangani kwa upande wao wamesema wana imani kubwa na Hailu kutokana na rekodi yake ya utendaji uliotukuka, hasa katika nyanja za elimu, afya, na miundombinu. 

Wamesema kuwa uamuzi wake wa kurejea kuwania nafasi hiyo ni fursa nyingine ya kuendelea kuona maendeleo ya haraka na yenye tija katika eneo lao.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com