Mkuu wa Kitengo cha Malipo katika Benki ya CRDB, Madaha Chabba, ambaye pia ni mtaalamu mahiri wa masuala ya fedha na uchumi, leo Juni 28,2025 amejitokeza kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kishapu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Madaha amewasili mapema kabisa asubuhi katika ofisi za CCM Wilaya ya Kishapu, ambapo baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo amesema amejitosa ili kutumia uzoefu wake kuinua maendeleo ya wananchi wa Kishapu.
“Nina nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Kishapu kwa maarifa na weledi nilionao katika sekta ya fedha, uchumi na usimamizi wa rasilimali. Natambua changamoto zilizopo na nina suluhisho la kweli,” amesema Chabba.
Social Plugin