Wadau wa usawa wa kijinsia kutoka maeneo mbalimbali nchini wakifuatilia moja kwa moja 'Mubashara' Hotuba ya Bajeti ya Taifa ya mwaka 2025/2026 iliyowasilishwa leo Alhamisi, Juni 12, 2025 bungeni Dodoma na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba. Tukio hilo limefanyika katika jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’ lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam, likiwa na lengo la kujadili Bajeti hiyo kwa jicho la kijinsia na kuangazia namna inavyogusa mahitaji ya wanawake, vijana na makundi mengine pembezoni. Picha na Kadama Malunde

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2025/26, bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2025/26, bungeni jijini Dodoma.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wadau kutoka sekta mbalimbali nchini wamekutana leo Alhamisi, Juni 12, 2025, katika jukwaa maalum la ‘Kijiwe cha Kahawa’ lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), kwa ajili ya kufuatilia na kujadili Hotuba ya Bajeti ya Taifa ya mwaka wa fedha 2025/2026 iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba.
Jukwaa hilo limefanyika katika ukumbi wa TGNP uliopo Mabibo, jijini Dar es Salaam, limewakutanisha wadau wa maendeleo kutoka mashirika ya kiraia, wanaharakati wa masuala ya kijinsia, wachumi, vijana, na wakilishi wa makundi maalum, kwa lengo la kujadili kwa kina namna bajeti hiyo inavyogusa mahitaji ya kijinsia na haki za kijamii.
Akizungumza wakati wa kufungua jukwaa hilo, Kaimu Mkurugenzi wa TGNP, Bi. Clara Kalanga, amesema kuwa jukwaa la ‘Kijiwe cha Kahawa’ ni sehemu muhimu ya ushiriki wa wananchi katika mchakato wa uchambuzi wa sera na bajeti ya Serikali kwa jicho la kijinsia.
“Tunataka kuona bajeti inakuwa nyenzo ya kuleta usawa – sio tu kiuchumi bali pia kijamii. Ni muhimu kuona namna inavyowagusa wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na makundi yaliyoko pembezoni,” amesema Bi. Kalanga.
Washiriki wa jukwaa hilo wamefuatilia mubashara hotuba ya bajeti kupitia matangazo kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kisha kushiriki mijadala kuhusu athari na fursa zinazotokana na bajeti hiyo, hususan kwa makundi yaliyokuwa yakipaza sauti zao kwa muda mrefu kuhusu masuala ya afya, elimu, ajira, na ustawi wa jamii.
Kwa miaka kadhaa sasa, TGNP imekuwa ikiendesha majukwaa kama haya kama njia ya kuongeza uwazi na ushirikishwaji wa kijinsia katika mchakato wa kupanga na kutekeleza bajeti ya taifa, ikiweka msisitizo kwenye maendeleo jumuishi na endelevu kwa wote.
Kaimu Mkurugenzi wa TGNP, Clara Kalanga, ambaye ni Mkuu wa Programu - TGNP, Clara Kalanga akifungua Mjadala katika jukwaa la 'Kijiwe cha Kahawa' lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ajili ya kujadili Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa mtazamo wa kijinsia uliofanyika katika ukumbi wa TGNP Jijini Dar es salaam

Mwenyekiti wa TGNP, Bi. Gemma Akilimali akizungumza wakati akifunga mjadala katika jukwaa maalum la ‘Kijiwe cha Kahawa’ lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), kwa ajili ya kufuatilia na kujadili Hotuba ya Bajeti ya Taifa ya mwaka wa fedha 2025/2026 iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Washiriki wakiwa katika jukwaa la 'Kijiwe cha Kahawa' lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ajili ya kujadili Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa mtazamo wa kijinsia, wakifuatilia mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi iliyowasilishwa Bungeni Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.
Washiriki wakiwa katika jukwaa la 'Kijiwe cha Kahawa' lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ajili ya kujadili Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa mtazamo wa kijinsia,wakifuatilia mubashara Hotuba ya Hali ya Uchumi iliyowasilishwa Bungeni Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.

Social Plugin