Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC MTATIRO ASHIRIKI SIKU YA MAONYESHO YA VIPAJI NA UBUNIFU KWA WANAFUNZI (CAREER FAIR) CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI _ KIZUMBI (KICoB) AAHIDI KUANDAA KONGAMANO LA VIJANA


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, ameongoza maadhimisho ya siku ya maonyesho ya vipaji na ubunifu kwa wanafunzi ( career fair) chuo kikuu cha ushirika Moshi tawi la Shinyanga Kizumbi( KICoB)

Akizungumza na wanafunzi wa Chuo Cha KICoB Mei 16,2025 katika viwanja vya Chuo hicho Wakili Mtatiro ameeleza kufurahishwa kwake na kiwango cha ubunifu na maarifa yaliyooneshwa na wanafunzi wa KICoB kupitia maonesho ya kazi zao, vipaji vya sanaa, burudani, na ubunifu wa utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.

Wakili Mtatiro amesema tukio hilo limethibitisha kuwa vijana wa Tanzania wana uwezo mkubwa ambao unahitaji kuendelezwa kwa dhati ili kuisaidia nchi kufikia malengo yake ya maendeleo endelevu.

Akitambua umuhimu wa malezi ya kizalendo na maendeleo ya vijana kitaifa, Wakili Mtatiro amewahakikishia wanafunzi hao kuwa ataandaa kongamano maalum la vijana, litakalowakutanisha kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga, likiwa na lengo la kuwaelimisha juu ya masuala ya uzalendo, ubunifu, ujasiriamali, na uwajibikaji katika jamii.

“Vijana ni hazina ya taifa letu. Tukiwapa mwongozo sahihi katika taaluma na maadili, tutakuwa tumeliwekea taifa msingi imara wa maendeleo. Nitahakikisha tunakuwa na kongamano la vijana litakalowajengea uwezo wa kujitambua, kuwa wabunifu na kuwa raia wema wanaowajibika,” amesema Wakili Mtatiro.

Aidha, ametoa pongezi kwa wakufunzi wa KICoB pamoja na Serikali ya Wanafunzi (MoCUSO) kwa maandalizi mazuri ya tukio hilo muhimu na kuwasihi waendeleze utamaduni huo kila mwaka kwa kuwa unachochea ari ya ubunifu, mshikamano, na kujiamini kwa wanafunzi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Isaac Kazungu, amemshukuru mgeni rasmi kwa kutenga muda wake kushiriki tukio hilo muhimu na akaahidi kuendelea kushirikiana na uongozi wa Serikali ya Wanafunzi kuhakikisha Career Day inakuwa sehemu ya kalenda rasmi ya matukio ya chuo. Katika hafla hiyo, washiriki mbalimbali wamepata fursa ya kuonesha vipaji vyao huku washindi wa maonesho na mashindano mbalimbali wakiibuka na zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu na zawadi za heshima, kama njia ya kutambua juhudi zao.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, ameongoza maadhimisho ya Siku ya Career Day katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akipongeza kamati ya maandalizi ya Siku ya Career Day katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB)

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akikaribishwa na uongozi wa KICoB kwa ajili ya kushiriki Siku ya Career Day.

Maonesho ya ya bidhaa zinazo tengenezwa na wanafunzi wa KICoB.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akishuhudia ubunifu wa wanafunzi walioshiriki Siku ya Career Day.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akishuhudia ubunifu wa wanafunzi walioshiriki Siku ya Career Day.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akishuhudia ubunifu wa wawanafunzi walioshiriki Siku ya Career Day.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akishuhudia ubunifu wa wawanafunzi walioshiriki Siku ya Career Day.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akishuhudia ubunifu wa wawanafunzi walioshiriki Siku ya Career Day.
Vibe la Wanafunzi walioshiriki Siku ya Career Day.


TAZAMA MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA SIKU YA Career Day CHUO CHA KICob HAPA Chini.


































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com