
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dkt. Batilda Burian amesema bila kuwa na watanzania wenye afya nzuri kiakili na kimwili mustakabali wa nchi unaweza kuwa kwenye mashaka.
Akizungumza kwenye mbio za Tanga kwanza Jogging zilizoshirikisha vilabu vya ndani na nje ya Mkoa wa Tanga, Mkuu huyo wa Mkoa ameitaka jamii kupenda michezo na kuwa timamu kiafya.
“Lakini nimefurahi pia kuona watoto ambao wamekuja na wazazi wao jambo hilo ni nzuri kwa kuwa tutakuwa tunawarithisha watoto wetu,”alisema Balozi Dkt Batilda Buriani.“Kwa hakika uwakilishi huu mkubwa ni ishara ya kwamba nyinyi wanamichezo mnashirikiana ,Joging club sasa hivi zimekuwa ni taasisi kubwa ambazo zimekuwa na umoja na mshikamano,”anasema mkuu huyo wa Mkoa wa Tanga.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanga Kwanza Joging Club Mbaraka Rajabu amewahamasisha wananchi kujiunga na mbio hizo kwa ajili ya kuimarisha afya zao.“Mbio hizi ni umri wowote uwe mtu mzima uwe mtoto mbio hizi unaziweza ,hizi sio zile mbilo za marathoni ambazo zinahitaji mwendo mkubwa sana ,ni mbio za polepole kwa hiyo tunahamasisha kila mmoja ajiunge“Tukiwa kama Aviocean tumeamua kuidhamini Tanga Joging Club kutoka na umuhimu wa mchezo huu kwa afya za watanzania ,mbio hizo zinatusaidia miili yetu kuwa imara na kuwa na uwezo wa kuhimili magonjwa ,”anasema Ismail Maroki-Mkurugenzi wa Aviocean Company Limited,wadhamini.Ismail anasema hatua hiyo pia wanaifanya wakimuunga mkono Mh Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameonesha umuhimu wa michezo kwa ajili ya kuboresha afya za watanzania.Naye wananchama wa Club ya Korogwe Joging Fitness Club Getrude Mlawa amesema toka ajiunge na club hiyo afya yake imeanza kuimariska akitolea mfano wakatii ambao alikuwa na unene wa kupithsa ,laini sasa afya yake inaridhisha na mwili wake unauwezo wa kufanya jambo lolote bila shaka
Social Plugin