Wakili Petter Madeleka
Na Hadija Bagasha Tanga
WAKILI Peter Madeleka ameiandikia barua ofisi ya msajili msaidizi wa nyaraka mkoa wa Tanga akimuomba kuondoa pingamizi lililowekwa kwenye kiwanja Plot namba 7 kilichopo Raskazone jijini Tanga kutekeleza amri ya mahakama.
Madeleka ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga mara baada ya kufika kwenye ofisi ya Msajili Msaidizi wa Nyaraka mkoani Tanga kwa ajili ya kufanya upekuzi na kujua hadhi ya kiwanja hicho.
Wakili huyo amesema pingamizi hilo liliwekwea mwaka 2014, na wakala wa Majengo Tanzania (TBA) zuio ambalo mahakama iliamuru kuondolewa baada ya kubaini kuwa halikuwa na sababu ya msingi ya kuwepo kwenye kiwanja hicho.
“Kwa mujibu wa sheria zuio lolote linalowekwa baada ya mwaka mmoja linakwisha muda wake, lakini zuio hili licha ya mahakama kuamuru liondolewe bado ofisi ya Msajili Msaidizi wa Nyaraka inaendea kulitambua na mteja wangu kwa sasa hawezi kufanya kitu chochote kwenye eneo hilo,”amesema Madeleka.
Madeleka amesema haada ya mteja wake kufika mahakama kuu kanda ya Tanga na baadae mahakama ya rufani ya Tanzania na uamuzi kutoka wa kuondolewa kwa pingamizi hilo ,hatua itakofuata ni kupeleka jambo hilo kwa Muheshimiwa Rais ambaye kwa sasa ndiye anayeweza kutoa kauli juu ya jambo hilo.
Social Plugin