Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YANGA NA JKT KUTELEZA UWANJA WA MKWAKWANI MEI 18, MABORESHO MAKUBWA YAMEFANYIKA


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

KUELEKEA katika mchezo wa nusu fainali wa Crdb Federation Cup unatarajiwa kuchezewa Mei 18, katika Uwanja wa Ccm Mkwakwani jijini Tanga, maboresho makubwa yamefanyika uwanjani hapo.

Akizungumza uwanjani hapo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ustaadhi Rajab Abdulrahman amesema kama chama ambacho kina dhamana ya uwanja huo ni kwamba upo tayari kwa ajili na maboresho hayo bado yanaendelea katika baadhi ya maeneo.

Amesema hapo awali uwanja huo ulikuwa na changamoto katika eneo la kuchezea lakini kutokana na juhudi za uongozi wa Ccm MKoa, Chama cha Mpira wa miguu nchini (TFF) kupitia Rais wa Walles Karia waliona juhudi hizo na kuunga mkono katika maboresho hayo.

"Awali kulikuwa na majani ambayo hayakufaa kuchezea, tukipata uamuzi wa kuondoa udongo na majani yote tukaweka haya ya sasa ambayo yanafaa zaidi na sasa hivi uwanja upo vizuri, hakuna tena visingizio,

"Na kwa kushirikiana na TFF tumeshaandaa michoro ya kubadilisha muonekano mzima wa uwanja huu, tumejipanga kufunga viti, kuweka jukwaa la kisasa lakini pia vyumba vya kubadilisha nguo kwa wachezaji" amesema Ustaadhi Abdulrahman.

Sambamba na hayo amebainisha kwamba CCM kwenye suala zima la sanaa, burudani na michezo, inakuwepo katika kila ilani ya uchaguzi na ni endelevu na wanahakikisha wanaitekeleza kwa vitendo.

"Tunachokifanya hapa, haya ni maelekezo kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha kwamba michezo hii ya mpira wa miguu inadumishwa sana" ,amefafanua.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com