
Kwa sasa mimi ni Mama wa watoto wawili ambao nawapenda sana kutokana na mazingara ambayo nilipitia hadi kuwapata, kuna wakati nawatazama watoto wangu na kujikuta machozi yakinitoka.
Si machozi ya uchungu bali machozi ya furaha, ni kitu ambacho kila siku nashukuru maana naona kwangu ni zaidi ya miujiza.
Ukisema uchungu wa mwana aujuaye mzazi, basi mimi nahisi uchungu huo naujua mimi kuliko mwanamke yeyote yule, naona kama nimepitia changamoto sana katika uzazi wangu.
Social Plugin