Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. BITEKO AWASILI NCHINI MOROCCO KWA ZIARA YA KIKAZI



Na Mwandishi wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi inayolenga kukuza na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili katika Sekta ya Nishati.

Mara baada ya kuwasili, Dkt. Biteko amepokelewa na Naibu Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu nchini humo, Mhe. Mohamed Ouhmed, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na mwakilishi katika eneo la Morocco, Mhe. Ali Jabir Mwadini.

Akiwa nchini humo, Dkt. Biteko anatarajiwa kukutana na kuzungumza na mwenyeji wake Waziri wa Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Mhe. Leila Benali ambapo watajadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Nishati.

Dkt. Biteko ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dennis Londo, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa nishati vijijini (REA), Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com