Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

OJADACT WAHUDHURIA KIKAO CHA BAJETI WIZARA YA HABARI



Taasisi ya kihabari inayosaidia Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya nchini (OJADACT) imehudhuria usomwaji wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya uongozi wake Profesa Paramagamba Kabudi sambamba na wasaidizi wake ambao ni Naibu Waziri Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa.

Uwasilishwaji na upitishwaji wa bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, umefanyika Mei 7, 2025 bungeni jijini Dodoma.Mbali na OJADACT iliyowakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa OJADACT
na Mratibu wa Kampeni ya Kaziinaongea Fatma Jalala, taasisi za kihabari nyingine zilizohudhuria na kuwakilishwa na wakuu wa taasisi hizo ni;

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura; Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, Mwenyekiti wa MISA Tanzania (MISA-Tan), Edwin Soko, Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (JOWUTA), Caren-Tausi Mbowe, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TEF, pamoja na Mhariri Mkuu mstaafu wa Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com