
BARAZA la Masheikh mkoani Tanga, limeandaa kongamano la kimataifa la kusoma Quran (Tawhid) ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi.
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Sharifu Muhannah Ahmad ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa ushirikiano wa Masheikh mkoani Tanga, alisema kongamano hilo litafanyika Mei 24 mwaka huu kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Sharifu Muhannah alisema kongamano hilo litakalojuisha wasoma Koran kutoka ndani na nje ya Tanzania,
Alitakuwa na watu 13,000 watakaoshindana Kusoma Tawhid.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya TAMTA Shamsiyah, Mohamed Abduh Dhikiri, alisema kongamano hili litakaloanza saa 8:000 asubuhi hadi saa 6:00 mchana litahushuriwa na wasomaji wa Kimataifa.
Naibu Mudir wa taasisi ya Shamsiyah Sheikh Ramani Mabruk alisema umuhimu wa kongamano hilo ni kuwaunganisha watu wawe kitu kimoja kuhakikisha kwamba kitabu cha Koran kimeletwa na Mungu kuwaunganisha pamoja.
"Kongamano hilo litakuwa na faida nyingi kwa Jamii licha ya kuwaunganisha lakini mungu ameleta kitabu cha Koran ili kikae katika nyoyo za waumini wake," alisema Sheikh Mabruk.
Mudir wa taasisi ya Kiislamu ya Ali bin Abi Talib, Sheikh Mohamed Zuber aliwaomba waislamu na wasiokuwa waislamu kuhudhuria kwa wingi kongamano hilo ambalo pia litatumika kuombea amani ya nchi na viongozi wake.
Alisema kutakuwa na wasomaji kutoka nchi za Pakistan, Uingereza na sehemu nyingine za Dunia na wanaungana na Sheikh Mkuu wa Tanzania Muft Abubakar Zuber kuwaalika wananchi katika kongamano hilo ili kufanikisha usomaji huo wa Koran.
"Sisi kama waja wa Mungu tutakuwa katika hali gani katika siku hiyo ambayo itakuwa na umuhimu mkubwa na faida kwa watu wote," alisema Sheikh Zuber.
Social Plugin