Mechi hiyo imechezwa mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza kuishangilia Stand United, wakitoka uwanjani wakiwa na furaha baada ya ushindi muhimu.
Mchezo huo uliovuta mashabiki wengi wa soka wa Kanda ya Ziwa ulianza kwa kasi, ambapo Stand United walitawala mchezo kwa vipindi vyote viwili na kufanikiwa kuzifumania nyavu za Geita Gold mara mbili.
Goli la kwanza la Stand United lilipatikana katika dakika ya 14 kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji Yusuph Adam.
Kipindi cha pili kilishuhudia Geita Gold wakijitahidi kusawazisha, lakini safu ya ulinzi ya Stand United iliendelea kuwa imara.
Katika dakika ya 85, Stand United walipata penati baada ya mchezaji wao kuchezewa vibaya ndani ya eneo la hatari.
Omary Rajabu aliyepewa jukumu la kupiga penati hiyo hakufanya makosa, na kuandika bao la pili kwa Stand United kwa mkwaju safi na wa kujiamini.
Kwa matokeo haya, Stand United wanaendelea kujikita vizuri kwenye mbio za kupanda daraja kuelekea Ligi Kuu ya NBC Premier League, huku Geita Gold wakitakiwa kurekebisha makosa yao kabla ya mechi zijazo.
Social Plugin