
Na Lydia Lugakila _ Missenyi
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amewataka wananchi kuwaanika hadharani waharifu wanaofanya dhulma kwenye jamii zao ikiwa ni pamoja na wale wanaofanya unyanyasi unaoambatana na ukatili.
Waziri Ndumbaro ametoa kauli hiyo April 15, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa kata Nsunga wilayani Missenyi mkoani Kagera Dk Ndumbaro ambapo amewata Wananchi kuwa wawazi ili kuwaanika waharifu kupitia kampeini ya msaada wa kisheria anbayo haitaacha changamotoo yoyote inayohusu maswala ya kisheria.
“Muda wa kuwataja waharifu hadharani ni sasa, baadhi ya watu ni wanyanyasaji, wengine wamenyanganya watu ardhi ,kunyanyasa wajane, ubakaji na ulawiti, nataka kuwahakikishia wananchi kuwa kampeni haitaacha changamotoo yoyote inayohusu sheria sisi tunasema ni haki,usawa na maendeleo,” amesema Ndumbaro.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Frankilini Rwezimula amesema huduma za kisheria kupitia kampeni hiyo itadumu katika Wlaya ya Missenyi kwa siku 9 ambapo kila siku timu itasikiliza kero na changamoto za kisheria vijiji vitatu kwa siku ,ndani ya Kata kwa siku moja.
“Naomba wananchi tujitokeze kwa wingi kuleta kero zetu za kisheria ili zipate ufumbuzi ,lakini sio kero tu hata Elimu ya kisheria kujua swala lako litaenda wapi lakini pia serikali inakusaidia kupata wanasheria watakakusaidia kupata majawabu ya haki zao ,tusiwe wakimya kwa mambo yanayotuumiza,” amesema Rwezimula.

Naye Mbunge wa Jimbo la Nkenge Frolent Kyombo amesema kuwa uwepo wa kampeni hiyo ni tunu na fursa kwa wananchi wa Missenyi kwani wananchi wengi hawana uwezo wa kujiwekea wanasheria na kuwaghamia.
Ameswma anaamini wananchi wa Missenyi kupitia kampenu hiyo watatatua changamotoo zao zinazowakabili ,kwani baadhi ya wananchi kesi zao zimeshindwa kuendelea kutokana na kutokuwa na gharama za kuwalipa mawakili ambapo amewahakikishia wananchi wa Missenyi kuwa kampeni hiyo ya kisheria inamajawabu yao yote hivyo wasikose kujitokeza.
Ameishukuru serikali kwa kujenga jengo la mahakama katika Wilaya ya Missenyi kwani wananchi wengi wanyonge walikuwa hawana uwezo wa kusafiri kwenda mahakama ya wilaya ya Bukoba ,hivyo uwepo wa mahakama ndani ya wilaya hiyo ni sehemu ya wananchi kupata haki kutokana na chombo hicho kutoa haki kwa kila mtu.


Social Plugin