Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara,Dkt Hashil Abdallah,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa 20 wa Makatibu Wakuu wa Biashara wa Mkataba wa eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) ambao ulikuwa na lengo la kutathimini utekelezaji wa Mkataba huo unaofanyika jijini Kinshasa,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt Hashil Abdallah amewashauri Makatibu Wakuu wa Biashara chini ya Mkataba wa eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) kuhakikisha wanaakisi matarajio ya wananchi na kuendana na maono mapana ya Ajenda ya 2063 ya Afrika tunayoitaka.
Dkt. Abdallah ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano huo ametoa agizo hilo April 11, 2025 wakati akifungua Mkutano wa 20 wa Makatibu Wakuu wa Biashara wa AfCFTA ambao ulikuwa na lengo la kutathimini utekelezaji wa Mkataba huo unaofanyika jijini Kinshasa,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Aidha Dkt Abdallah amesema Nchi Wanachama, Sekretarieti ya AfCFTA, na wataalamu waeendelee kutimiza wajibu wao thabiti katika kusukuma mbele ajenda ya AfCFTA.
Dkt. Abdallah amebainisha kuwa utekelezaji wa Mkataba huo ulioanza rasmi 1 Januari 2021, umepiga hatua kubwa, hususan katika kuhama kutoka kwenye mazungumzo hadi utekelezaji wa vitendo.
Amesema kupitishwa kwa nyaraka za Kisheria za awamu ya Pili ya majadiliano na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali ya Umoja wa Afrika ni uthibitisho wa dhamira ya pamoja ya kuhakikisha AfCFTA inafanikiwa.
Dkt Abdallah pia amesema majadiliano yao katika siku chache zijazo yatakuwa na mchango mkubwa katika juhudi za kukamilisha majadiliano ya maeneo ambayo hayajakamilika, kuboresha mikakati na kutoa mapendekezo thabiti kwa Waheshimiwa Mawaziri katika Mkutano wao wa 16 wa Baraza la Mawaziri.
Amesema mafanikio ya AfCFTA si tu kuhusu sera na makubaliano ya kisheria, bali yanahusu kubadilisha mazingira ya uchumi wa Bara la Afrika na Kupitia juhudi zinazolenga, kuimarisha biashara ndani ya Afrika, kukuza viwanda, kuongeza ajira, na kujenga uchumi imara. 

Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji ,Bi.Aziza Mumba,akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kifedha na kibiashara yaliyoandaliwa leo Aprili 12,2025 na taasisi ya Chama wa Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) kwa wanawake 200 wanaojihusisha na ujasiriamali mkoa wa Dodoma.

Rais wa Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA),,Bi. Fikira Ntomola,,akizungumza wakati wa mafunzo ya kifedha na kibiashara kwa wanawake 200 wanaojihusisha na ujasiriamali mkoa wa Dodoma leo Aprili 12,2025.

Sehemu ya washiriki wakifatilia mafunzo ya kifedha na kibiashara yaliyoandaliwa na taasisi ya Chama wa Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) kwa wanawake zaidi ya 200 Mkoa wa Dodoma wanaojihusisha na ujasiriamali.

Sehemu ya washiriki wakifatilia mafunzo ya kifedha na kibiashara yaliyoandaliwa na taasisi ya Chama wa Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) kwa wanawake zaidi ya 200 Mkoa wa Dodoma wanaojihusisha na ujasiriamali.


Sehemu ya washiriki wakifatilia mafunzo ya kifedha na kibiashara yaliyoandaliwa na taasisi ya Chama wa Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) kwa wanawake zaidi ya 200 Mkoa wa Dodoma wanaojihusisha na ujasiriamali.


Sehemu ya washiriki wakifatilia mafunzo ya kifedha na kibiashara yaliyoandaliwa na taasisi ya Chama wa Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) kwa wanawake zaidi ya 200 Mkoa wa Dodoma wanaojihusisha na ujasiriamali.


Wakichangia
.....
ZAIDI ya wanawake 200 wanaojihusisha na ujasiriamali mkoani Dodoma wamepatiwa mafunzo ya kifedha na kibiashara yaliyoandaliwa na taasisi ya Chama wa Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA), ikiwa ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa wanawake wajasiriamali utakaofanyika Aprili 13,mwaka huu jijini Dodoma.
Akifungua mafunzo hayo leo April 12, 2025 jijini Dodoma Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji ,Bi.Aziza Mumba,amesema kuwa mafanikio ya wajasiriamali wanawake yanategemea nidhamu ya fedha na matumizi sahihi ya maarifa ya kifedha.
“Biashara haiwezi kukua kama hakuna nidhamu ya fedha. Mafunzo haya ni muhimu kwa kila mjasiriamali anayetaka kuimarika kiuchumi katika Mkoa wa Dodoma ,” amesema Bi. Mumba
Aidha ameeleza kuwa benki nyingi ziko tayari kutoa mikopo, lakini zinahitaji kuona mwelekeo wa biashara na usimamizi mzuri wa mapato na matumizi ya mjasiriamali husika.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA),,Bi. Fikira Ntomola, amesema kuwa taasisi hiyo ilianzishwa mwaka jana kwa lengo la kuinua wanawake kiuchumi kupitia elimu ya fedha, uwekezaji, na usimamizi wa biashara.
“Tunahamasisha wanawake kuwekeza kwenye masoko ya mitaji na kuhakikisha wanakuwa na bima ya biashara zao kama kinga dhidi ya majanga,” amesema Bi. Ntomola.
Mafunzo hayo yamehusisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya fedha, wakiwemo wawakilishi wa benki waliotoa elimu kuhusu mikopo, marejesho, na fursa za kifedha zinazopatikana kwa wanawake wajasiriamali.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Mkoa wa Dodoma, Bi. Mary Barnabas, amesema kuwa wanawake waliopata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo ni sehemu ndogo ya zaidi ya wanawake 6,000 wanaojihusisha na ujasiriamali mkoani humo.
“Tunapaswa kuzingatia elimu tunayopewa. Tukiitumia vyema, biashara zetu zitakua na mitaji itaongezeka,” amesema
Pia amesisitiza umuhimu wa wanawake kubadili tabia za kifedha, kuepuka matumizi yasiyopangwa kwenye bajeti, na kutumia rasilimali walizonazo kwa malengo ya maendeleo ya biashara.
Mafunzo hayo, yaliyoambatana na kauli mbiu “Huduma Jumuishi za Kifedha”, yamelenga kuwawezesha wanawake kupata mikopo kwa urahisi, kukuza mitaji yao, na kulinda biashara kupitia uwekezaji na bima.
Social Plugin