Na Hamida Kamchalla, TANGA.
WANANCHI Mkoa wa Tanga wamesema wamefarijika sana kwa ujio wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo walielezea furaha matamanio yao.
Wamesema kubwa walichofurahia ni jinsi Rais anavyopambana kuleta maendeleo mkoani humo ikiwa ni pamoja na kuomba kuongezeka Wakala wa kuleta meli ili kupata ajira zaidi ambapo pia itaongeza mapato.
"Tunashukuru kwa mama kututembelea hapa Tanga lakini pia kwa maboresho yanayoendelea kwenye bandari yetu, kikubwa ambacho tunatamani na tunaomba kwa mama, Wakala wa meli waongezeke ili vijana wetu wapate ajira kwa wingi" ,amesema Eveline Mshana.
"Tumefurahi sana Rais wetu kututembelea, kuboreshwa bandari hii tunapata ajira hivyo tunaomba wawekezaji waje kwa wingi ili ajira ziongezeke pia maendeleo ya Mkoa wetu yawe mazuri" ,amesema Aisha Mkamba.
Leo Machi 1, 2025, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemaliza ziara kwa kutembelea katika bandari ya Tanga ambapo alikagua maboresho ya gati mbili mpya.
Social Plugin