Na Barnabas Kisengi, Kibakwe-Mpwapwa
Mwenyekiti wa jumuia ya Uvccm Mkoa wa Dodoma Comred Abdulhabib Japhar Mwanyemba Leo hii amefanya ziara ya kikazi katika Jimbo la Kibakwe na wananchi wa Jimbo hilo huku akianzia katika Kijiji Cha Iyenge kwa kufungua tawi la Uvccm Iyenge na baada hapo aliekea makao makuu ya Jimbo Kibakwe na kuzungumza na wananchi.
Katika hotuba yake Mwenyekiti Mwanyemba amewasisitiza wananchi wa Jimbo la Kibakwe kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa George Simbachawene ambae ni mbunge jimbo hilo pamoja na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani wao ndio wanaoshirikiana kwa pamoja kuwaletea wananchi wa Jimbo la Kibakwe na Tanzania kwa ujumla.
Ziara hiyo ya Mwenyekiti imeambatana na wajumbe wa Kamati kuu ya utekelezaji mkoa wakiongozwa Wensilaus Mazanda ambae pia ni Katibu wa hamasa na chipukizi mkoa wa Dodoma pamoja na Mwenyekiti Uvccm wilaya ya Mpwapwa Comred Yohana Malogo pamoja na Katibu wa Uvccm wilaya ya Mpwapwa Comred Mengi Mwakisole na wajumbe wengine na viongozi kutoka serikali ya Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa
Social Plugin