
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, amewataka wanasiasa kuacha kutumia mfungo wa Ramadhani kujinufaisha kisiasa kwa kutumia kigezo cha kuandaa futari.
Akitoa salamu za heri kwa waum
ini wa dini ya kiislamu na wakristo katika kipindi cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kwarezima, Macha amesema kipindi hiki ni muhimu kwaajili ya kumkaribia mwenyezi Mungu kwa toba kama zilivyo Imani za waamini hao hivyo wanasiasa wasitumie kipindi hiki kukidhi haja zao za kisiasa kwa kutenda mambo yenye asili ya rushwa.
Aidha amewaomba waumini wa dini ya kiislamu na wakristo kutumia kipindi hiki cha mfungo kuombea taifa na watu wake hususani kuelekea kipindi uchaguzi mkuu ili kuwe na uchaguzi huru na haki ikiwa ni pamoja na kutumia sadaka zao kuwakumbuka waliopungukiwa na kuwafikia wahitaji.
Katika hatua nyingine amewataka wafanyabiashara kwenye masoko kuacha kujinufaisha kupitia kipindi hiki kwa kupandisha bei za mahitaji sokoni ili kuifanya funga kuwa nzuri ma yenye tija.
Social Plugin