
Meneja wa Ngara Farmers kutoka Ngara Mkoani Kagera Elisha Mathias
Na Lydia Lugakila - Ngara
Ili kunufaika na zao la Kahawa ni lazima ubora wa zao hilo uzingatiwe ili wewe mkulima na pia mwenye kampuni ya ununuzi wa zao hilo anufaike ni kama walivyofanya Ngara Farmers hadi kuibuka na tuzo ya mshindi wa kwanza katika uzalishaji bora wa zao hilo Afrika.
Chama cha Msingi cha Wakulima wa Ngara (NGARA FARMERS AMCOS LTD) wameshinda tuzo ya mshindi wa kwanza kwa wazalishaji bora wa kahawa aina ya Robusta Africa kwenye mashindano ya African Fine Coffees Competition yaliyoandaliwa na African Fine Coffees Association(AFCA)
Mashindano hayo yamefanyika Februari 28, 2025 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere International Cofference Center jijini Dar Es Salaam na yalilenga Makampuni,Vyama vya Ushirika na Wakulima wa zao la kahawa kwa Nchi 25 za Africa upande wa Robusta na Arabica kwa kushindanisha kahawa za wakulima kwa kutambua kahawa bora ambapo yamehusisha majaji kutoka Nchi mbalimbali ikiwemo Rwanda,Kenya, Afrika kusini na Uganda.
Akizungumza na Malunde 1 blog Meneja wa Ngara Farmers Elisha Mathias amesema kuwa ili kunufaika na zao la Kahawa lazima kutumia njia mbali mbali ili kufikia mafanikio zaidi.
Amesema kuwa wao kama Ngara Farmers wamefanikiwa kupitia kutoa elimu kwa wakulima kabla na baada ya kuvuna ambapo faida za kuvuna kahawa iliyoiva na kukomaa kwani ndio chanzo cha bei ya Mkulima kuwa bora, kushirikiana na ofisi ya Kilimo ya Wilaya na maafisa ugani wa kata na vijiji kupitia mashamba ya wakulima mara kwa mara hasa kuona shughuli za utunzaji wa mashamba ya wakulima wakati wa msimu na wakati usio wa msimu jambo linalowasaidia wakulima kuwashauri namna bora ya utunzaji wa mashamba yao na namna ya kupambana na changamoto za mashamba hasa magonjwa na ukame kipindi mvua ikiwa changamoto ili kuja kuvuna kahawa bora.
Mathias ameongeza kuwa njia nyingine ya kuzingatia ubora wa kahawa ni wakati wa makusanyo hasa vituo vya ukusanyaji kwa kumwaga chini na kukagua kahawa ya Mkulima yote kabla ya karani kuipokea na kama haijafikia kiwango cha unyevu (12.5)karani anamshauri Mkulima arudi nayo nyumbani aianike vizuri na Mjumbe wa zamu kituo husika atafatilia zoezi hilo kama limefanyika kwa Mkulima huyo na kuhakikisha kahawa unarudi kwenye chama,kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa wakulima wanaovuna kahawa mbichi na changa kwa lengo la kuwahi kujipatia kipato.
"Mfano kwa kushirikiana na Ofisi ya Afisa Ushirika wilaya Ngara na Afisa Kilimo wilaya na Serikali za vijiji msimu uliopita tulichukulia sheria wanachama zaidi ya 10 kwa kufanya makosa hayo ya kuvuna kahawa mbichi na changa kwa kuwatoza faini ya ya kulipa fedha ikiwa ni pamoja na kuwafuta uachama ili kuwa fundisho kwa wakulima wengine na ilisaidia sana kwani mchezo huo ulikoma" ,amesema Mathias.
Meneja huyo aliongeza kuwa Chama kina wafanyakazi wa kitengo cha Uthibiti ubora wa zao ambapo shughuli yao kubwa ni kuhakikisha kinaendelea kutoa elimu kwa Mkulima na kutambua changamoto za Mkulima na sababu za uvunaji kahawa changa na mbichi lakini pia zoezi la kuanika chini kwenye udongo na kutatua changamoto hizo kwa kuwawezesha turubai baadhi ya wakulima ili kuzingatia ubora wa uanikaji na magunia na kuzingatia ubora wa uvunaji katika vyombo safi lakini zaidi utunzaji wa kahawa katika mazingira safi makavu na salama na kutokuchanganywa na mazao mengine au mifugo wakati wa utunzaji.
Hata hivyo Meneja huyo amehimiza vyama vya ushirika kufika katika Ofisi hizo kwa ajili ya kubadilishana mbinu bora ili kumkwamua Mkulima wa zao la Kahawa hasa katika nafasi ya ubora inayomuongezea thamani ya zao lake
Social Plugin