Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA MGENI RASMI SIKU YA MARIDHIANO ARUSHA



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano (JMAT), Alhajdi Mussa Salum, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kitaifa ya maridhiano,
******


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Maridhiano (JMAT), Alhajdi Mussa Salum, amewaasa Watanzania kuungana kupinga udini, ukabila na chuki katika jamii, hatua itakayosaidia kukuza amani na mshikamano nchini.


Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kitaifa ya maridhiano, ambapo pia alieleza kuwa mambo mbalimbali ya kijamii yatafanyika, ikiwemo kutembelea wafungwa na uchangiaji damu ili kuendelea kuimarisha mshikamano katika jamii.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa JMAT, Mchungaji George Fupe, amesema maridhiano ni jambo muhimu katika kulinda amani nchini, na jumuiya hiyo itaendelea kusimamia kikamilifu suala hilo ili kujenga jamii imara yenye mshikamano.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji, Dkt. Peter Rashid, amesema amani ndiyo msingi wa mafanikio katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, huku akiwahimiza viongozi wa dini mbalimbali na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki maadhimisho hayo.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yatakayofanyika Februari 26 Jijini Arusha anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji, Dkt. Peter Rashid,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kitaifa ya maridhiano
Makamu Mwenyekiti wa JMAT, Mchungaji George Fupe,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kitaifa ya maridhiano

PICHA ZOTE NA JAMES SALVATORY 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com