Mkuu wa majeshi Jenerali Jacob John Mkunda akimvisha nishani Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed mkoani Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob John Mkunda baada ya kuvishwa nishani hizo Mkoani Ruvuma
Mkuu wa majeshi Jenerali Jacob John Mkunda akimvisha nishani alizotunukiwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed akiwa amesimama imara wakati wa kwenda kuvishwa nishani hizo alizotunukiwa
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa jeshi
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa jeshi leo Mkoani Ruvuma
Na Regina Ndumbaro Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ametunukiwa nishani nne na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hafla hiyo ya kihistoria imefanyika leo mkoani Ruvuma mbele ya maafisa wa jeshi na askari wa Kanda ya Kusini.
Tuzo hizo zimekuja kama ishara ya kutambua mchango mkubwa wa Kanali Ahmed Abbas Ahmed katika utumishi wa umma na mchango wake katika kuimarisha usalama na maendeleo ya mkoa wa Ruvuma.
Katika hafla hiyo, viongozi mbalimbali wa kijeshi waliohudhuria, wakishuhudia tukio hilo muhimu.
Akizungumza mara baada ya kupokea nishani hizo, Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameonesha furaha kubwa na kueleza kuwa ni heshima kubwa kwake kutambuliwa kwa mchango wake.
Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuthamini juhudi zake na kumpa nafasi ya kuendelea kulitumikia taifa kwa moyo wa uzalendo.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amemshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, pamoja na maafisa wote wa jeshi na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliokuwa sehemu ya tukio hilo.
Amesema kuwa nishani hizo ni motisha kwake kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.
Tukio hilo limeonesha mshikamano mkubwa kati ya viongozi wa serikali na taasisi za ulinzi na usalama, jambo linalothibitisha dhamira ya serikali ya awamu ya sita katika kuthamini na kutambua mchango wa viongozi na watumishi wa umma wanaojitoa kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Wananchi wa Ruvuma wamepokea taarifa hizo kwa furaha, wakiona ni ishara ya uongozi bora unaoendelea kusimamia maendeleo na ustawi wa jamii katika mkoa huo.
Social Plugin