Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC WAIGONGA TABORA UNITED 3-0

Simba SC imeendelea kutawala Ligi Kuu Bara baada ya kuifunga Tabora United kwa magoli 3-0 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. 

Ushindi huu umewawezesha kufikisha pointi 43, na hivyo kupita Yanga ambayo ina pointi 42, huku timu zote zikiwa na michezo 16.

 Leonel Ateba alifunga magoli mawili, na Shomari Kapombe alifunga moja, wakichangia kwa kiasi kikubwa kuiletea Simba ushindi huu muhimu.

Kwa upande mwingine, Tabora United, ambayo iliifunga Yanga 3-1, inabaki na alama 25, ikikalia nafasi ya tano katika msimamo wa ligi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com