TIC YAKUTANA NA WAWEKEZAJI WATANZANIA KAGERA, YAHAMASISHA UWEKEZAJI



Na Mbuke Shilagi Kagera.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeendesha semina kwa wawekezaji Watanzania Mkoani Kagera ambapo kimeeleza umuhimu na faida za kuwekeza ndani ya Tanzania hasa Mkoa wa Kagera.

Akizungumza katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera uliopo Manispaa ya Bukoba, Ambapo kimehudhuriwa na wafanyabiashara, wawekezaji wazawa wa Mkoa wa Kagera Kutoka wilaya mbalimbali pamoja na kiongozi Kutoka chuo Kikuu Cha Dar es salaam, Mkuu wa idara ya uhandisi, Kilimo chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dk. Arnold Towo amesema kuwa kupitia uwekezaji kutatengeneza ajira kwa vijana lakini pia kuwajengea uwezo, ujuzi na ufahamu mkubwa wa kutengeneza miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii.

''Kupitia uwekezaji tunajenga na kukuza walipa kodi wadogo wakati na wakubwa ambao baada ya miradi yao kukamilika na kusimama wataanza kulipa kodi na kunufaika lakini pia kupitia uwekezaji tunalenga kutengeneza bidhaa bora na bidhaa hizo  zitauzwa ndani na nje ya nchi'', amesema.

Aidha amesema kuwa sio miradi yote inasajiliwa na kituo cha uwekezaji Tanzania na kusema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha B kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya uwekezaji Tanzania sura namba 38 iko miradi minne isiyosajiliwa na kituo ambayo ni miradi ya madini, utafutaji wa mafuta na gesi {utafiti}  na miradi ya ujenzi wa viwanda vya kemikali hatarishi , silaha na vilipuzi.

Pia amesema kuwa jukumu hilo la kuhamasisha na kusimamia uwekezaji katika nchi ya Tanzania halisimamiwi na kituo cha uwekezaji Tanzania TIC pekee ila zipo tasisi zingine ambazo zimeundwa na serikali ambazo zinashiriki pia kuifanikisha  lakini pia kuitengeneza ambapo ni IPZA,Tume ya madini,ZIPA, TIC na PPP.

'' Tunapoongelea nchi yetu ni nchi ya uwekezaji hoja ya kwanza nchi yetu ni ya amani na utulivu kwanini amani na utulivu? sisi ni nchi ya kidemokrasia na ni nchi ambayo tayari imeshuhudia mabadiliko sita ya uongozi na tuko awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini pia tangu tupate uhuru katika nchi yetu hatukuwahi kupata machafuko wala kuingia katika matatizo makubwa ya vita na mwekezaji wa nje na hata wa ndani kikubwa anachoangalia ili kufanya maamuzi ya kuwekeza ni uwepo wa amani'',amesema.

Sambamba na hayo amesema kuwa mchakato na utaratibu wa kusajili mradi ni pamoja na cheti cha usajili wa kampuni ambazo zote zinasajiliwa na BRELA ambao ni sehemu ya kituo cha huduma kwa wawekezaji mahala pamoja lakini pia katiba ya kampuni na fomu ambayo inatakiwa kujaza na inawezekena kujazwa kwa mfumo wa kidijitali kupitia simu pia kuwa na andiko fupi la nini unaenda kufanya pia na ushahidi wa mtaji wa kuwekeza na muhimu zaidi ni bodi na unasajili.

''Kama ni mwekezaji raia wa nje au ni mtanzania anayeingia ubia na wawekezaji kutoka nje katika kutekeleza mradi kiwango cha chini kabisa cha mtaji ni fedha za Tanzania zisizopungua dola laki tano lakini kama mwekezaji ni mtanzania kiwango cha chini cha mtaji ni fedha za Tanzania zisizopungua dora elfu 50 takribani Tsh. 125 milioni'' amesema.

''Ikiwa ni mwekezaji mahiri {strategic inversters} kutoka nje kiwango cha chini cha mtaji ni fedha za Tanzania zenye thamani ya dola milioni 50 na ikiwa ni mtanzania ni kiwango kisichopungua fedha za Tanzania zenye thamani ya dola milioni 20''

''Wawekezaji mahiri maalum {special strategic inversters} ambao wao ni wenye mtaji usiopungua fedha za Tanzania zenye thamani ya dola milioni 300'', amesema Dk. Arnold Towo.

Kwa upande wake Alhaji Shakiru Yahaya Kyetema maarufu Dangote wa Muleba amewashukuru TIC kwa elimu na semina waliyoitoa huku akiomba semina nyingine waje na watu wengine ambao ni TRA, Idara ya uhamiaji na mabenki ili wajue changamoto zilizopo na ziweze kutatuliwa.

''Serikali inabidi kwenye mkutano mwingine nimewashauri wakija watu wa TIC waambatane na watu wote wahusika wa mabenki, Idara ya uhamiaji, TRA ili kusudi sisi wafanyabiashara tunaojitoa muhanga wa kuwekeza na wale watu tuzungumze mambo ambayo yanaweza  lkutusaidia ili serikali au TIC iweze kushirikiana na kutupa nguvu ya kutupunguzia mzigo'' amesema Dangote wa Muleba.


Kaimu katibu tawala Mkoa wa Kagera Bw. Isaya Tendega akizungumza katika semina ya TIC na wawekezaji wazawa Mkoani Kagera 
Prof. Nelson Boniface Naibu Makamu wa Mkuu wa chuo - utafiti akiwa katika semina ya TIC na wawekezaji wazawa Mkoani Kagera 
Mkuu wa idara ya uhandisi, Kilimo chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dr. Arnold Towo 
Alhaji Shakiru Yahaya Kyetema maarufu Dangote wa Muleba Mwekezaji mzawa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post