DC MTATIRO AKAGUA UJENZI MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MADARAJA...AAGIZA MKANDARASI ANYANG'ANYWE MRADI WA DARAJA MANISPAA YA SHINYANGA

 


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro amefanya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja Manispaa ya Shinyanga, huku akiagiza Mkandarasa Kampuni ya Fomast anyang'anywe ujenzi wa daraja kutokana na utendaji wake kazi kutoridhisha.

Mtatiro amefanya ziara hiyo leo Julai 8,2024 akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Shinyanga,na Watalamu kutoka Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA).

Mtatiro akizungumza kwenye ziara hiyo,amewataka Wakandarasi watekeleze miradi yao kwa wakati na ubora,na kwamba wale ambao ni wazembe hawatapewa kazi,huku akiagiza Mkandarasi kutoka Kampuni ya Fomast anyang'anywe kazi ya ujenzi wa daraja na kubaki na barabara kutokana na utendaji wake kazi kutoridhisha.

"Mkandarasi huyu ambaye anatekeleza ujenzi wa barabara na daraja kuunganisha Kata ya Mwawaza na Chibe, naagiza kazi ya daraja anyang'anywe apewe mtu mwingine yeye abaki na barabara tu, na Jumamosi nipewe mpango kazi wake wa ukamilishaji wa barabara hii,"amesema Mtatiro.
"Tunakagua miradi hii ya maendeleo ili kuona fedha ambazo zinatolewa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan namna zinavyofanya kazi,hivyo kwa Wakandarasi ambao ni wazembe hatutafanya nao kazi," ameongeza.

Katika hatua nyingine Mtatiro, ameagiza utaratibu mzuri ufanyike namna ya kuwaelemisha wanannchi na kuwaondoa ambao wanafanya shughuli za kilimo kwenye mto ning'wa eneo ambalo litajengwa daraja hivi karibuni.
Kaimu Meneja wa (TARURA)wilaya ya Shinyanga Mhandisi Yohana Williamu, amesema Mkandarasa Kampuni ya Fomastick kazi zake niza kusuasua na wamekuwa wakizungunza naye kumhimiza kuongeza kazi lakini bado hali iko vilevile huku akiahidi kutekeleza maagizo ya kumtaifisha kazi ya ujenzi wa daraja ambalo alikuwa bado kuanza.

Kwa upande wake Mkandarasi kutoka Kampuni ya Fomast Exavel Mapunda,akijitetea amesema kwamba ameshindwa kuendana na kasi ya ujenzi kutokana na kukabiliwa na changamoto ya mvua.
Aidha,barabara na madaraja zilizokaguliwa ni ile ambayo inaunganisha Kata ya Mwasele na Ndala, Kata ya Mwawaza na Chibe hadi kwenda Oldshinyanga, Butengwa,pia barabara za Majengo mapya,pamoja na katikati ya mji ambazo zenyewe zinajengwa kwa kiwango cha Lami.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇


CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post