RC MACHA ACHAFUKWA UCHAFU MWINGI MANISPAA YA KAHAMA, ...MABANGO YA MIRADI YAANDIKWE KISWAHILI'

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya mkoani Shinyanga kuchukua hatua kwa wanaochafua barabara na mitaro ya kupitishia maji kwa kutupa chupa huku akiitaja Manispaa ya Kahama kuongoza kwa uchafu.

Mhe. Macha amesema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Julai 15,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

“Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri chukueni hatua kwa wanaochafua barabara. Mfano tuna haja ya kuufanyia usafi Mji wa Kahama, Mji wa Kahama ni tatizo kubwa, ni mchafu. Tunayo kazi ya kuanza kusafisha Mji wa Kahama, mitaro ya maji imejaa chupa na hakuna maji yanayotembea maana yake wananchi wa maeneo hayo ndiyo wanahusika. Kahama si safi ni lazima tuchukue hatua. Manispaa ya Kahama badilikeni, tunzeni mazingira na muimarishe usafi wa mazingira,amesema Mhe. Macha.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.

“Serikali imeleta fedha nyingi kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya barabara ni lazima tutunze miundombinu ya barabara, tutunzeni barabara hizi, haiwezekani Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kusuka Kamba halafu kuna mtu mwingine anachoma hiyo Kamba. Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Wabunge, Madiwani na viongozi mbalimbali tuweke mpango mzuri wa kusafisha barabara zetu”,ameongeza Mhe. Macha.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga amepongeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro kwa kupambana na wakandarasi wazembe katika wilaya ya Shinyanga huku akiipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa utunzaji bora wa miundombinu ya barabara lakini pia kwa kuendelea kuwa Manispaa safi kitaifa na amezitaka halmashauri zingine kwenda kujifunza katika Manispaa hiyo.
Aidha Mhe. Macha ameagiza Lugha ya Kiswahili itumike kwenye Miradi yote ya ujenzi wa barabara ili kuendelea kukuza Lugha ya Kiswahili.

“Miradi yote inapotambulishwa iandikwe kwa lugha ya Kiswahili. Mabango yote yanayotambulisha miradi, yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili ili kukuza Kiswahili ", amesema Macha.

Katika hatua nyingine Macha amekemea tabia ya wananchi kujimilikisha maeneo ya hifadhi za barabara ambapo Manispaa ya Kahama pia inaongoza kwa wananchi kuvamia maeneo ya hifadhi za barabara na kufungua biashara.

“Kahama ni shida kubwa, wananchi wamejimilikisha hifadhi za barabara na wamefungua biashara zao. Mamlaka za Maji na TANESCO msipeleke huduma za maji na umeme mahali pasipo sahihi mfano kwenye hifadhi za barabara kwani kufanya hivyo mnahamasisha wananchi kuingia kwenye maeneo ya hifadhi. Endapo tutaruhusu wananchi wajenge kwenye hifadhi za barabara basi kuwe na mikataba”,amesema.

“Hali kadhalika bado kuna udhaifu katika usimamizi wa Wakandarasi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu, tuendelee kuwasimamia wakandarasi wafanye kazi kwa viwango na kwa wakati na Wakandarasi hawa tusiwape kazi nyingi, tusiwape vipande vingi”,ameeleza.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema bado kuna changamoto ya kuharibika kwa taa za barabarani, magari kuzidisha uzito hali inayochangia kuharibika kwa barabara.

Hata hivyo Mhe. Macha amepongeza Meneja wa Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga kwa utekelezaji mzuri wa miradi kwa maelekezo ya serikali.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa ametaka changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi zitatuliwe mapema lakini pia uzalendo uimarike katika kusimamia miradi ili fedha zinazoletwa na Mhe. Rais Samia zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuwaletea maendeleo wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Akichangia hoja wakati wa kikao hicho, Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo amesema ni wajibu kwa wataalamu kuhakikisha maazimio yanatolewa kwenye vikao yanatekelezwa kwa wakati badala ya kutoa majibu ya zimamoto wakati vikao hivyo akashauri Maazimio yaandikiwe taarifa ndani ya muda mfupi ili utekelezaji ufanyike kwa wakati ili kutatua changamoto kwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo.

Aidha ameipongeza TARURA na TANROADS kwa kazi nzuri wanazofanya hivyo kuwaomba waongeze kasi zaidi licha ya kuwepo kwa changamoto upande wa Manunuzi na baadhi ya Wakandarasi kutokuwa na uwezo.

Mhe. Butondo ameeleza kuwa miradi ya ujenzi wa barabara imekuwa ikichelewa kutokana na baadhi ya Wakandarasi kutokuwa na vifaa vya ujenzi lakini wengine hawana uwezo wa kujenga miradi hali inayosababisha miradi ichelewe kutekelezwa.

“Mkandarasi katika mji wa Mhunze ni kama hayupo, kazi haifanyiki kabisa, tunataka ujenzi wa Km 2 za barabara katika mji wa Mhunze ufanyike, tunataka mji wa Mhunze upendeze....utaratibu wa kuwaangalia hawa wakandarasi uangaliwe , baadhi yao hawana uwezo, hawana vifaa vya ujenzi matokeo yake miradi inakwama. Tuwabaini wakandarasi wenye uwezo ili kazi zikamilike kwa wakati kwa viwango vinavyotakiwa”,ameongeza Mhe. Butondo.

"Ujenzi wa Barabara ya Kolandoto - Mhunze na Mwangongo katika kiwango cha lami wa urefu wa Km 20 tumepewa shilingi Bilioni 2 za kuanzia katika bajeti ya mwaka huu 2024/2025 , tunaomba barabara hii ianze kujengwa kutokana na kwamba wananchi wamekuwa wakiihitaji barabara hii ijengwe, ujenzi huu uanze haraka ili tuwapunguzie wananchi adha ya barabara....Pia tunapoweka Moramu kwenye baadhi ya barabara tusiwe haya mawe makali yanayoleta adha kwa wananchi kwenye baadhi ya vipande vya barabara",amesema Butondo.
Mhe. Emmanuel Cherehani.

Naye  Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani ameomba kuongezwa kwa barabara za lami Ushetu lakini pia Mameneja wa TARURA waliokuwa kwenye Halmashauri tatu za wilaya  ya Kahama warudishwe na barabara ambazo hazina mitaro ziwekewe mitaro.

Meneja wa Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Samwel Mwambungu amezitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na wizi wa alama za barabarani, taa nyingi zinagongwa,ufinyu wa bajeti kwenye matengenezo na mifumo ya manunuzi (Nest) kuwa katika matengenezo.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Samwel Mwambungu.

Akiwasilisha taarifa ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2023/2024 amesema walitengewa kiasi cha fedha Sh.10.6, lakini wakapokea Sh.bilioni 5.5 hadi kufikia Juni 30.

Mhandisi Mwambungu amesema kwa upande wa miradi ya kimkakati ambapo uwanja wa Ndege Ibadakuli hadi sasa ujenzi wa eneo la kurukia ndege umefikia asilimia 70 na jengo la abiria asilimia 30, na kwamba barabara ya Kolandoto hadi Mhunze tayari wameshatengewa fedha kuanza ujenzi kilomita 20, huku barabara ya Oldshinyanga- Solwa upembuzi yakinifu ukiwa tayari umekamilika.

Naye Meneja wa Wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) mkoani Shinyanga Mhandisi Avith Theodory amesema moja ya changamoto wanazokumbana nazo ni uwezo mdogo wa Wakandarasi hali inayosababisha washindwe kufanya majukumu yao ipasavyo.
Meneja wa TARURA mkoani Shinyanga Mhandisi Avith Theodory 

Mhandisi Theodory amekiri kwamba uwezo mdogo wa wakandarasi kutekeleza miradi ya barabara ni tatizo na kubainisha kwamba watawasiliana kwenye bodi ambayo hua inawasajili sababu wakija kuomba zabuni na kuonyesha “CV”huonekana wako vizuri lakini kumbe hana uwezo.

Akiwasilisha taarifa ya mpango wa bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwamba walitengewa kiasi cha fedha Sh.bilioni 18.2 lakini wakapokea Sh.bilioni 5.7, huku katika mwaka wa fedha 2024/2025 wakitengewa Sh.bilioni 16.6.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 15,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 15,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 15,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 15,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 15,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa ShinyangaMkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 15,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 15,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 15,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 15,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 15,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) mkoani Shinyanga Mhandisi Avith Theodory akitoa taarifa kwenye kikao hichoMeneja wa Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Samwel Mwambungu akitoa taarifa wakati wa kikao hicho
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze akitoa taarifa kuhusu mradi wa TACTIC wakati wa kikao hicho
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Masudi Kibetu akitoa taarifa kuhusu mradi wa TACTIC wakati wa kikao hicho
Kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga kikiendelea

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post