NHIF YATUMIA MAONYESHO YA 11 YA BIASHARA NA UTALII KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU VIFURUSHI VYAO


Afisa Uanachama wa NHIF Mkoa wa Tanga kushoto akitoa elimu kwa diwani wa Kata ya Usagara Jijini Tanga wakati alipofika kwenye Banda lao

 Na Oscar Assenga, TANGA

 

MFUKO wa Taifa wa Bima  ya Afya Tanzania (NHIF) Mkoani umeshirikia maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara ili kutoa elimu kuhusu huduma wanazotoa ikiwemo vifurushi  wanavyovitoa.

 

Banda la Mfuko huo limekuwa lililopo kwenye maonyesho hayo limekuwa ni kivutio kwa wananchi ambao wamefika kupima afya zao na kupata ushauri namna ya kuepukana na magonjwa yasiyoyakuambikizana.

 

Pia wananchi hao wamekwenda kwa ajili ya kuona namna ya kujiunga na vifurushi mbalimbali vinavyotolewa na mfuko huo ili kuweza kunufaika na matibabu bure pindi wanapougua.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post