RC MTANDA AFUNGUA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA...DCEA & THPS WATOA ELIMU KWA WANANCHI

Na Kadama  Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amefungua Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kitaifa  leo Juni 28, 2024 katika viwanja vya Nyamagana, jijini Mwanza.

Maadhimisho hayo yatafikia tamati Juni 30,2024 ambapo Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho hayo akitarajiwa kuwa Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza wakati akifungua Maadhimisho hayo yanayoongozwa na Kauli mbiu “Wekeza kwenye kinga na tiba dhidi ya dawa za kulevya”, Mhe. Mtanda amewakaribisha wakazi wa mkoa wa Mwanza na maeneo jirani kujitokeza katika maadhimisho hayo ambapo pia watapata fursa ya kupewa elimu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya.

Amesema tatizo la dawa za kulevya limezidi kuongezeka hivyo pia kuchangia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na kwamba ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anapiga vita uuzaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya.

Mhe. Mtanda amesema Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kupambana na dawa za kulevya ikishirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) na wadau waliowekeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

"Hongereni sana Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kazi nzuri mnayofanya katika kudhibiti uuzaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya. Mmeonesha dhahiri kuwa mmejipanga vizuri kutekeleza majukumu yenu. Ni wajibu wa wadau mbalimbali kushirikiana na DCEA kupiga vita dawa za kulevya",amesema Mhe. Mtanda.

Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) ni miongoni mwa wadau wanaoshiriki maadhimisho hayo ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya kwa kutoa elimu kuhusu Huduma za tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya zinazotolewa kwenye vituo vya Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT).

THPS inatekeleza afua ya huduma ya Tiba kwa waraibu (MAT) katika mikoa ya Pwani na Tanga kupitia mradi wa Afya Hatua inaoutekeleza kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) kupitia Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (US. CDC).

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda akizungumza wakati akifungua Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kitaifa Jijini Mwanza leo Juni 28, 2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda akizungumza wakati akifungua Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kitaifa Jijini Mwanza leo Juni 28, 2024

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kitaifa Jijini Mwanza leo Juni 28, 2024

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda (kulia) akitembelea Banda la Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) wakati akifungua Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kitaifa Jijini Mwanza leo Juni 28, 2024

Mfamasia kutoka Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Monica Maliganya (kulia) akitoa elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na THPS, VVU na UKIMWI, elimu kuhusu Huduma za tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya zinazotolewa kwenye vituo vya Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) kwa wananchi waliotembelea banda la THPS wakati wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Mwanza.

Mnufaika wa huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya kupitia kituo cha huduma za MAT kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga – Bombo kinachowezeshwa na THPS kwa kushirikiana na Serikali, bi. Mariam Semwaza akitoa elimu ya kipimo cha kujipima VVU mwenyewe (Self Test) kwa wananchi waliotembelea banda ya THPS wakati wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Mwanza.

Wananchi wakiwa katikaBanda la Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post