BANDA LA UTPC LAWAVUTIA WENGI KWENYE MAONESHO YA IDODOMIA INTERNATIONAL EXPO


Wakazi wa Dodoma na viunga vyake wameendelea kutembelea kwenye Banda la maonesho la Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania ambapo maonesho makubwa ya Kimataifa ya  fursa za uwekezaji, utalii, michezo na utamaduni yanaendelea katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Dodoma vilivyopo mkabala na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari ni sehemu ya wadau mbalimbali katika maonesho hayo ambapo katika banda hilo wanaonesha na kueleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Umoja huo ikiwa ni pamoja na miradi inayotekeleza kwa mustakabali wa maendeleo ya sekta ya habari na jamii kwa ujumla. 

Pamoja na mambo mengine, Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania wamegawa vitu mbalimbali ikiwemo machapisho, vitabu vya kihabari, vijitabu vinavyoeleza maana ya UTPC, kalamu na majarida. 

Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania ni asasi mwamvuli inayosimamia Klabu za Waandishi wa Habari 28 zilizopo nchi nzima.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post