HOTELI MPYA 'AZAT HOTEL' YAZINDULIWA RASMI TINDE


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amezindua hoteli mpya 'AZAT HOTEL'  iliyopo katika kata ya Tinde wilayani Shinyanga .

Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika Juni 1, 2024 katika viwanja vya hoteli ya AZAT HOTEL vilivyopo jirani na kituo cha mzani wa Tinde wilayani Shinyanga.


Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi mmiliki wa AZAT HOTEL Mhe. Azza Hilal Hamad amewakaribisha wateja kwenda kujipatia huduma bora zinazotolewa hotelini hapo.


"AZAT HOTEL ni sehemu sahihi kwa ajili ya kupumzika kwa wageni na hata wenyeji, huduma zitakazotolewa hapa AZAT HOTEL ni pamoja na malazi na chakula kwa gharama nafuu kabisa, vyumba vyetu ni bora, rafiki na vyenye viwango bora, lakini pia mbali na kutoa huduma hii ya hoteli tunajihusisha na ukodishaji wa Tents kwa ajili ya shughuli mbalimbali, karibuni sana ukifika hapa Tinde hoteli ni moja tu AZAT HOTEL kwa mawasiliano zaidi unaweza kutupigia kupitia simu namba 0742 565 555", amesema Mhe. Azza Hilal Hamad.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amepongeza uwekezaji uliofanywa na Azza Hilal Hamad kwa kuthamini wageni na kuongeza mapato, uchumi na maendeleo kwenye halmashauri hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana vyema na wawekezaji.

"Hongera sana dada yetu Azza Hilal Hamad kwa uwekezaji uliyoufanya kwenye kata hii ya Tinde ukizingatia ni miongoni mwa maeneo yanayopokea wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali, niseme tu ni hatua kubwa kwako kama mwanamke, kama serikali tunaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wawekezaji hususani sekta binafsi, niwahakikishie wakazi wa maeneo haya kuwa ile changamoto ya bei kubwa ya maji ukilinganisha na maeneo mengine sasa imekwisha, nimeshaongea na viongozi husika kwenye sekta ya maji na kuanzia sasa bei itakuwa sawa na maeneo mengine" , amesema Wakili Julius Mtatiro. 

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude ambaye alikuwa mgeni mualikwa katika hafla hiyo amempongeza Mhe. Azza Hilal Hamad kwa kutoa ajira kwa vijana kupitia ujenzi wa hoteli hiyo na kuwasihi vijana kufanya kazi kwa bidii pindi wapatapo nafasi na kutoa wito kwa jamii kushirikiana vyema na wawekezaji ili kuwatia moyo waendelee kuwekeza kwenye maeneo yao.

"Sisi tunakupongeza sana wewe na familia yako kwa jitihada hizi, hatuna budi kushirikiana na wawekezaji kama hawa ili kuwatia moyo waendelee kuwekeza kwenye maeneo yetu, na kutoa nafasi kwa vijana wetu ili waweze kujikwamua kiuchumi", amesema DC Mkude.


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Zoezi la kukata utepe kuashiria uzinduzi kwenye hoteli ya AZAT HOTEL.

TAZAMA PICHA MUONEKANO WA AZAT HOTEL

Muonekano wa nje hoteli ya AZAT HOTEL.
Baadhi ya watu waliohudhuria kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa hotel ya AZAT HOTEL.
Mhe. Azza Hamad akiwaonesha wageni muonekano na huduma za hoteli hiyo. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post