BABA AMUUA MTOTO WAKE KIKATILI, AMNYOFOA VIA VYA UZAZI, MKE AMUANGAMIZA MMEWE USINGIZINI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP. Alex Mkama

Na Christina Cosmas, Morogoro

JESHI la Polisi Mkoani Morogoro linamshikilia Erick Julias (33) mkazi wa Miembeni wilayani Kilombero kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kufikia wa kiume mwenye umri wa miaka sita kwa kumnyofoa via vya uzazi pamoja na kukata viganja vyote viwili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP. Alex Mkama amesema tukio hilo limetokea June Mosi mwaka huu Wilayani Kilombero Mkoani Morogo.

Kamanda Mkama amesema mtuhumiwa huyo kabla ya kufanya unyama huo alimtenganisha  kichwa na kiwiliwili mtoto huyo.

Katika tukio jingine, Jovina Mwakiyee (33) mkazi wa kijiji cha Mang'ula A wilayani Kilombero anashikiliwa na Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kula njama na kumuua mume wake wa ndoa.

Kamanda Mkama amesema mwanamke huyo alipanga njama  na Kisha kumuua mwanaume wake aliyeitwa Christian Tangaraza  (39) ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi Signal .

Kamanda Mkama amesema tukio hilo lilitokea usiku wa June Mosi mwaka huu ambapo marehemu aliuawa kwa kupigwa na kitu butu wakati akiwa amelala ndani ya nyumba yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post