WANANCHI MAVANGA WAKATAZWA KULIMA, KUINGIZA MIFUGO KWENYE VYANZO VYA MAJI

 

Na Elizabeth John,       LUDEWA.


WANANCHI wa kijiji cha Mavanga wilayani Ludewa mkoani Njombe wametakiwa kutofanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na uingizaji mifugo kwenye vyanzo vya maji kwani hali hiyo itasababisha vyanzo hivyo kukauka.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Niombe Anthony Mtaka wakati wa ziara yake ya siku tatu ya kutembelea miradi wilayani Ludewa ambapo akiwa kijiji cha Mavanga wananchi walilalamikia uchafu wa maji ya bomba kwenye mradi unatekelezwa kijijini hapo wenye thamani ya zaidi ya bilioni 1.3 utakaohudumia  wakazi wapatao 5,000.


"Maji yanachafuliwa na shughuli za kibinadamu ,mtashikana uchawi bure lakini wachawi ni sisi wenyewe ,Mh Rais Samia Suluhu Hassan ameshatimiza wajibu wake fedha zimefika,wekundu wa maji unasababishwa na kuingiza mifugo ngo'mbe,"alisema Mtaka. 


Awali mmoja wa wananchi wa kijiji hicho Musa mwabena aliishukuru serikali kwa mradi huo lakini alilalamikia changamoto ya maji ya bomba kutoka yakiwa machafu hali ambayo inahatarisha afya zao.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post