POLISI SHINYANGA WAKAMATA PIKIPIKI 16, DAWA ZILIZOISHA MUDA, ALIYEMTAJA MTU MCHAWI ATUPWA JELA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata pikipiki 16 za wizi na zisizo na kadi, viroba 25 vya madawa ya kulevya aina ya Mirungi, Tv 01, Mzani 01, Redio 01, pombe ya moshi lita 20 pamoja na pakti 86 za dawa za binadamu zilizokwisha muda wa matumizi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Mei 27,2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema vitu hivyo vimekamatwa katika kipindi cha mwezi mmoja na wiki moja kuanzia Aprili 17, 2024 mpaka Mei 27, 2024 kufuatia Ushirikiana wa Jeshi la Polisi na Jamii katika kubaini na kutanzua uhalifu kwa kufanya doria, misako pamoja na Operesheni mbalimbali.

Katika kipindi hicho pia Jumla ya kes 15 zimepata mafanikio ambapo kesi 01 ya kuvunja nyumba usiku na kuiba mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka 01 na kesi moja ya kumtaja mtu mchawi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja.

"Kesi 01 ya kupatikana na bhangi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha kutumikia jamii miaka 03, kesi 01 ya kuvunja duka usiku na kuiba mshitakiwa amehukumiwa kifungo cha nje miezi 12, kesi 01 ya kupatikana na madawa ya kulevya mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha kutumikia jamii miaka 02, kesi 01 ya kutorosha mtoto mshtakiwa ameamriwa kulipa faini tsh 50,000/=, kesi 01 ya kupatikana na mirungi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 02 jela.

Kesi 05 za wizi washtakiwa wamehukumiwa kifungo kati ya miezi 03 hadi miaka 03 jela, kesi 01 ya kujeruhi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha mwaka 01, kesi 01 ya shambulio la kudhuru mwili mshitakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka 01, kesi 01 ya kutishia kuua kwa silaha panga mshitakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka 01",amesema Kamanda Magomi.

Kamanda Magomi amesema pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kikosi cha Usalama barabarani limefanikiwa kukamata jumla ya makosa 6320 ya Usalama Barabarani ambapo makosa ya magari ni 4847 na makosa ya bajaji na pikipiki ni1473 wahusika waliwajibishwa kwa kulipa faini za papo kwa papo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha dawa za binadamu zilizokwisha muda wa matumizi.
Muonekano sehemu ya dawa za binadamu zilizokwisha muda wa matumizi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akionesha pikipiki zilizokamatwa


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post