PROF. MKENDA : TUMEENDELEA KUIMARISHA UDHIBITI NA KUKUZA MATUMIZI SALAMA YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2024/2025.

***

”Serikali imeendelea kuimarisha udhibiti na kukuza matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwa kutekeleza yafuatayo:
imesajili vituo vipya 43 vya Mionzi ayonishi na kufikisha jumla ya vituo vya mionzi 1,386 vilivyosajiliwa na vituo vipya 42 vya mionzi isiyoayonishi na kufikisha jumla ya vituo vya mionzi isiyoayonishi 409 vilivyosajiliwa. 

Aidha, Serikali imesajili vyanzo vipya 36 vya mionzi na kufikia jumla ya vyanzo vya mionzi 1,647 vilivyosajiliwa

Serikali imetoa leseni 633 za kumiliki na kutumia vyanzo vya mionzi, uingizaji nchini wa vyanzo vya mionzi 95, utoaji nje ya nchi wa vyanzo vya mionzi 13 na safirishaji wa vyanzo vya mionzi ndani ya nchi 47; imepima viwango vya mionzi kwa wafanyakazi 1,980 wanaofanya kazi katika vyanzo vya mionzi katika vituo 429. Aidha, viwango vya mfiduo vilivyopokelewa katika miezi mitatu mfululizo vilianzia 0.1 hadi 3.2 millisievert (mSv), ambavyo viko ndani ya ukomo unaokubalika wa udhibiti", Prof Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post