Na Moshi Ndugulile Cape town
Bunge la Afrika linaendesha warsha kwa waandishi wa habari wa nchi za kusini mwa Afika,ambapo takribani washiriki kutoka nchi kumi za ukanda huo wanashiriki.
Warsha hiyo inafanyika jijini Cape town Nchini Afrika ya Kusini ikijumuisha
waandishi wa habari kutoka nchi za Tanzania,Lesotho,Msumbiji.Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC,Malawi, Zambia,Botswana,Eswatin, Namibia,na mwenyeji Afrika ya kusini.
Madhumuni ya warsha hiyo yanakwenda sanjari na malengo ya Bunge la Afrika katika hatua za kushughulikia changamoto zilizopo,katika ukanda huo na maeneo jirani.
Kwa kutambua umuhimu na mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika ustawi na maendeleo ya taasisi hiyo,warsha hiyo inafanyika ili kuongeza uwanda mpana wa uelewa wa washiriki juu ya shughuli za Bunge ikijumuisha mafanikio na namna inavyoshughulikia changamoto zilizopo.