WAHITIMU SUA WATAKIWA KUACHA KUBWETEKA WATUMIE TAALUMA ZAO


Baadhi ya wanachuo SUA
Makamu mkuu wa chuo SUA Prof. Raphael Chibunda akizungumza kwenye Mahafali ya 43 ya wanachuo.
Jaji Joseph Since Warioba akihudhurisha wanachuo

Na Christina Cosmas Morogoro

 WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wameaswa kuacha kubweteka bali wachape kazi huku wakitumia ujuzi wa taaluma wanazopata kutatua changamoto za kijamii zilizopo kwenye kilimo na mifugo huku wakikiwakilisha vyema chuo hicho ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa baraza la chuo hicho Mwanasheria Mkuu Mohamed Chande Othman alisema hayo jana kwenye mahafali ya 43 ya chuo hicho yaliyohudhurishwa zaidi ya wahitimu 700 na Mkuu wa chuo hicho Jaji Joseph Sinde Warioba na kufanyika mjini hapa.


Mwenyekiti huyo alisema SUA hufundisha masomo ya sayansi, kilimo na mifugo kwa nadharia na vitendo ambapo mhitimu akiitumia nafasi aliyoipata vizuri itamsaidia kupiga hatua katika kukamilisha kusudia lake la kuisaidia jamii kuinuka katika Nyanja zote muhimu ikiwemo Kilimo na Mifugo. 

Naye Makamu wa Mkuu wa chuo cha SUA upande wa taaluma, utafiti na ushauri Profesa Maulid Mwatawala aliwataka wahitimu kujenga dhana ya kutosubiri kuajiriwa bali wajiajiri na kutumia ubunifu walionao katika kutatua changamoto mbalimbali zilizopo nchini.
 

Profesa Mwatawala alisema iwapo watatumia ubunifu watafanikiwa kutoa elimu waliyoipata kwa wahitaji hata kabla ya kupata ajira na hivyo kukabiliana na changamoto zilizopo.


Naye Mmoja wa wahitimu wa chuo hicho Amina Malongo aliwashauri wahitimu wenzake kujenga tabia ya kujituma katika utekelezaji wa kazi zao jambo litakalowasadia kufikia malengo ya Kilimo yaliyopo nchini.

kupitia elimu aliyoioata anaweza kwenda kujiajiri na kutatua changamoto zinazowakumba wafugaji na wakulima. 

Alisema kwa kutumia elimu wanaliyoipata wana nafasi ya kujiajiri wenyewe na kujikita katika mambo mbalimbali muhimu ikiwemo ya ufugaji samaki, kilimo na kuendeleza ufugaji na kutatua changamoto za kilimo hasa kwa wakulima wadogo.

Awali Makamu wa mkuu wa chuo hicho Profesa Raphael Chibunda alisema chuo kinastahili kujipongeza kwa kuongeza idadi ya nguvu kazi yenye taaluma ujuzi na weledi kila mwaka ikiwa ni chachu ya kuongeza kasi ya maendeleo nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post