SILINDE: TUNAONESHA UMMA MABADILIKO CHANYA AMBAYO WIZARA IMEKUWA IKIYAFANYA KATIKA SEKTA YA KILIMO



Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amesema lengo la Wizara kuweka maonyesho katika viwanja vya Bunge ni kuonesha Umma mabadiliko chanya ambayo Wizara imekuwa ikiyafanya katika Sekta ya Kilimo kuanzia katika ngazi ya tafiti mpaka katika ngazi ya uwekezaji ya kuongeza thamani ya mazao.



"Tunaonesha watu namna ambavyo tunaendesha Sekta ya Kilimo Kidigitali yaani kwa kutumia vifaa vya kisayansi na teknolojia ikiwemo na namna ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali, wadudu waaribifu wakiwemo ndege na viuatilifu, kuangalia matumizi sahihi ya mbolea" ameeleza Mhe Silinde.


"Sisi wizara ya kilimo tunaamini kilimo katika njia ya kutumia sekta ya umwagiliaji (irrigation skims pamoja na mabwawa) tunaamini hii ndio inaweza kubadilisha sekta ya uchumi", ameongeza Mhe Silinde.


Maonesho hayo yamehudhuriwa na Wabunge mbalimbali pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Umma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post