BENKI YA TAIFA YA USHIRIKA MKOMBOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA

 
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb), amesema wizara yake kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika katika mwaka 2024/2025 itaratibu ukamilishaji wa kuanzisha Benki ya Taifa ya Ushirika kwa kuhamasisha vyama vya ushirika kuendelea kununua hisa ili kukamilisha mtaji hitajika wa Shilingi Bilioni 20. 

“Aidha, wizara imepanga kuwezesha uwekezaji katika mifumo ya kidigitali kwenye Vyama vya Ushirika na Mamlaka za Usimamizi, kuimarisha usimamizi na udhibiti wa Vyama vya Ushirika; kuwezesha vyama vya ushirika kujiendesha kibiashara na kuviwezesha kupata mitaji na kuhamasisha ushirika kwenye sekta mbalimbali na makundi maalumu.


"Wizara kupitia tume hiyo pia itaendelea kuimarisha matumizi ya mifumo ya Kidigitali katika kusimamia na kuendesha vyama vya ushirika. Katika mwaka 2024/2025 ambapo tume itanunua na kusambaza kompyuta mpakato 129 kwa Maafisa Ushirika ili kuwawezesha kutumia Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika,’ amesema Mhe. Bashe.


Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka 2024/2025, Mhe. Bashe amesema benki hiyo itaanza kwa kufungua matawi matatu katika Mikoa ya Dodoma, Mtwara na Kilimanjaro ambapo pia benki hiyo itawezesha Vyama vya Ushirika kupata mikopo na kuongeza mitaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post