DKT. TULIA , NAPE WAUMIZWA NA HALI YA UCHUMI WA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA

 

Na  Estomine Henry - Dodoma.

Imeelezwa kwamba changamoto ya kiuchumi inayovikabili Vyombo vya habari nchini, umeathiri hali ya ukuajia wa uhuru wa vyombo vya habari kwa kushidwa kujiendesha na vingine kusitisha shughuli zake.

Hayo yamebainishwa leo Mei 2,2024 jijini Dodoma katika Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Tanzania, ambapo Spika wa Bunge , Dkt. Tulia Akson,amesema,Uhuru wa vyombo vya habari unategemea uimara wa hali ya uchumi wa vyombo vya habari ili kuweza kukuza na demokrasia ya nchi.

Dkt. Tulia anasema, ili vyombo vya habari kuwa na uhuru ni vema changamoto ya kiuchumi ya vyombo vya habari kutatuliwa ili kuweza kukuza na kuendeleza demokrasia ya nchi.

" Ninaagiza taasisi  zote za serikali kuchukua hatua ya kulipa madeni yote ambayo wanadaiwa na vyombo vya habari na pia kuhakikisha  taratibu zinafanywa kwa ajili ya watumishi wa vyombo vya habari kulipwa Mishahara yao kama watumishi wengine",amesema  Dkt. Tulia.

Anasema , "Uchumi wa vyombo vya habari ukiwa duni una athiri hali ya ustawi wa demokrasia kwa kuwa baadhi ya vyama vya siasa hushindwa kugharamia vyombo vya habari na waandishi kipindi cha uchaguzi".

Vyombo vya habari ,Tanzania vinasherehekea  miaka 31 ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo habari huku vikiangaziwa kuzingatia maadili katika uchaguzi wa serikali za mitaa.


Aidha,Tulia amesema serikali iko tayari kupokea mrejesho kwa wadau wa habari juu changamoto  za kisheria zilizo kikwazo kwa vyombo vya habari ilizifanyiwe kazi.

"Bunge kupitia kamati yake ya masuala ya sheria itafanyia kazi baadhi ya vifungu vinavyo onekana kuwa ni changamoto kwa ustawi wa vyombo vya habari", amesema Dkt. Tulia.


Kwa upande wake ,Waziri wa Habari na Mawasiliano  Tanzania, Mhe.Nape Nauye amesema hali ya sasa ni nzuri tofauti na tulipotoka na suala llilopabaki ni changamoto ya uchumi wa vyombo vya habari.

"Hatujafika tunakotaka ila mabadiliko ni makubwa kwa serikali kushirikiana na vyombo vya habari na tumefanyia kazi maboresho ya sheria kadhaa",amesema Nnauye.

"Hatupo tulipokuwa jana kwa sasa  uhuru wa vyombo vya habari  unaimarika kila siku,vyombo vya habari vinafanyakazi na ukomavu umekuwepo kwa sekta ya habari ila  hatujafika tunapotaka kwenda",amesema Nnauye.

Naye ,Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania ,Deogratius  Nsokolo ameishukuru serikali kwa kufanya marekebisho ya vifungu vya sheria vilivyokuwa vina kandamiza uhuru wa vyombo vya habar Tanzania.

Waandishi wa habari Tanzania walikabiliwa na madhira kadha katika majukumu yao yaliyonyima uhuru wa habari kwa kipindi Cha miaka 10,Matukio yaliweza  kuishusha Tanzania katika sura ya kimataifa. 

Kwa mfano, katika ripoti za World Press Freedom Index, Tanzania iliendelea kushuka katika viwango vya uhuru wa habari kutoka nafasi ya 70 mwaka 2013 mpaka nafasi ya 124 mwaka 2021 na mwaka 2022 nafasi ya 123.

Takwimu za Baraza la Habari Tanzania za mwaka 2022,zilibainishwa taasisi zilizoongoza kwa matukio mengi dhidi ya uhuru wa habari ilikuwa ni polisi ambayo ilikuwa na matukio 51.

Wahusika wengine ni pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) matukio 21, wizara mbali mbali matukio 14, wakuu wa wilaya matukio tisa, mashabiki wa mpira matukio matano, wakulima na wafugaji  matukio mawili na watu wasiojulikana matukio kumi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post