SERIKALI YABAINISHA MPANGO WA KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI KUZALISHA BIDHAA BORA


NAIBU Waziri wa Viwanda na Biasha, Exaud Kigahe amebainisha mpango wa Serikali katika kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora ili kupata masoko ya uhakika.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Ester Malleko ambaye alitaka kujua mpango wa Serikali wa kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora na kupata masoko ya uhakika.

Akijibu swalin hilo, Kigahe alisema Serikali imeweka mipango kadhaa ya kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora ili kupata masoko ya uhakika ikiwa ni pamoja na kupitia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwasaidia wajasiriamali wadogo kupata maeneo/majengo ya kuzalishia bidhaa zao, kuwapatia mitaji kupita Mfuko wa NEDF na nembo ya ubora wa bidhaa zao kwa miaka mitatu bila gharama.

Amesema pia kupitia SIDO, TBS na Wakala wa Vipimo (WMA) kuendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali kuhusu kanuni za uzalishaji wenye tija, elimu ya utambuzi wa vifungashio na ufungashaji bora.

Pia amesema SIDO kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuendelea kuandaa na kuratibu maonesho mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwa ni sehemu ya kuchagiza ukuaji wa soko la bidhaa zinazozalishwa na Wajasiriamali.

Katika swali la nyongeza, Malleko alitaka kujua mpango wa serikali wa kufanya mapitia ya sera ya biashara na sera ya wajasilimali wadogo wadogo ambazo zimepitwa na wakati.

Pia alitaka mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wajasiriamali wanazalisha bidhaa zenye ubora.

Akijibu maswali hayo, Kigahe amesema ni kweli sera hizo zimepitwa na wakati na kuwa Serikali imeshaanza taratibu za mapitio ili ziweze kuendena na hali ya soko la ndani na nje na mahitaji ya sasa ya wajasiliamali.

Alisema pia Serikali imepanga kuweka mazingira mazuri kwa wajasiriamali ili kuweza kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango bora.

Kwa upande wa Mbunge wa Viti Maalum, Sophia mwakagenda alitaka kujua mkakati wa Serikali wa kuiwezesha SIDO ili kuweza kuwasaidia wajasiriamali wengi zaidi.

Akijibu wali hilo, Kigahe alisema SIDO imekuwa na uwezo mdogo wa kuwezesha mitaji kwa wajasiriamali ambao wamekuwa wakiongezeka kila wakati.

Amesema Serikali imeacha mchakato wa kuibadili sheria iliyoanzisha SIDO ili kuondoka kuwa taasisi ya uwezeshaji bali iweze kujiendesha kibiasharamae, sheria baada ya kuhudumia ianze kujiendesha kibiashara na kukidhi mahitaji ya wajasiliamali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post