RC MACHA AWATAKA WATUMISHI KUSIMAMIA VYEMA FEDHA ZA MIRADI, KUFANYA KAZI KWA UZALENDONa Marco Maduhu,KISHAPU

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,amezungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na kuwataka wachape kazi kwa Uzalendo katika kuwatumikia Wananchi pamoja na kusimamia vyema fedha za Miradi ya Maendeleo.

Kikao hicho na Watumishi wa Serikali kimefanyika leo Aprili 12,2024 katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, pamoja na kukagua baadhi ya Miradi ya Maendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa wilayani humo likiwamo Jengo la Ofisi ya Mkuu wa wilaya.
Amesema kila Mtumishi wa Serikali wilayani Kishapu,anapaswa kutekeleza wajibu pamoja na kufanya kazi wa Uzalendo na weledi Mkubwa katika kuwatumikia Wananchi na Taifa kwa Jumla, ikiwamo na kusimamia vyema fedha za utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.

"Sikuja hapa Kishapu kukutana na Watumishi kutoa Maonyo,wala kukemeana bali nimefanya kikao na ninyi kwa ajili ya kukumbushana juu ya utendaji kazi,fanyeni kazi kwa kutanguliza Uzalendo na kila Mtu atekeleze wajibu wake,"amesema Macha.
"Mimi nimekuja hapa Shinyanga kwa ajili ya kuendeleza kwa yale wenzagu walipoishia,pamoja na kutekeleza Maagizo ambayo nimepewa na Rais Samia,hivyo naombeni ushirikiano wenu na mfanye kazi kwa bidii,"ameongeza Macha.

Amewataka pia Watumishi kila Mmoja waheshimiane kwa nafasi yake, pamoja na kuacha kujiingiza kwenye Mahusiano ya kimapenzi ambayo mara nyingi yamekuwa yakivuruga ufanisi wa utendaji kazi.
Aidha,ameagiza pia maeneo yote ya Serikali yawekewe Mipaka zikiwamo Zahanati,Shule pamoja na vijiji vyote,ili kuondoa Migogoro ya mipaka kwenye uchaguzi.

Pia amekemea suala la vikundi hewa kwenye Mikopo ya Asilimia 10 ambayo itarudishwa hivi karibuni,bali iwafikie walengwa na kuwakwamua kiuchumi.
Katika hatua nyingine RC Macha amezungumza na Wazee wilayani humo, na kuwahakikishia Serikali itaendelea kuwatunza pamoja na kuwapatia huduma mbalimbali zikiwamo za Kiafya na upatikanaji wa Madawa ya Wazee.

Miradi ya Maendeleo ambayo imetembelewa na Mkuu wa Mkoa,ni Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Kituo cha Polisi, na Jengo la huduma jumuishi (One stop Center) Hospital ya wilaya ya Kishapu,ambapo pia alipita Ofisi za CCM wilayani humo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizunguma na Watumishi wa Serikali wilayani Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Wiliamu Jijimya akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapy Emmanuel Johnson akizungumza kwenye kikao hicho.
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Kikao kikiendelea.
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Kikao kikiendelea.
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungunza na Wazee wilayani Kishapu kwenye Ofisi yao.
Wazee wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akikagua Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kishapu.
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kishapu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akikagua ujenzi wa Kituo cha Polisi wilayani Kishapu.
Muonekano wa Jengo la Kituo cha Polisi wilayani Kishapu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akikagua Ujenzi wa Jengo la huduma Jumuishi (One stop Center) katika Hospital ya wilaya ya Kishapu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha (wapili kutoka kushoto) akiwa ziarani wilayani Kishapu akiambatana na viongozi mbalimbali (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post