MPANGO WA SERIKALI KUHAKIKISHA IFIKAPO MWAKA 2034 ASILIMIA 80 YA WATANZANIA WATATUMIA NISHATI SAFI
NAIBU KATIBU Mkuu wa Wizara ya Niashati James Mataragio amesema mpango wa Serikali ni kuhakikisha Tanzania ifikapo mwaka 2034 watanzania asilimia 80 watakuwa wanatumia matumizi ya nishati safi.

Mataragio aliyasema hayo leo mjini Tanga wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kwanza wa bajeti wa mwaka 2024 kati ya wabia wa maendeleo ya nishati pamoja na wakala wa nishati vijijini (REA) ambapo alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha watanzania wanapata nishati ya umeme kwenye maeneo yao na wakala huo umekuwa ukifanya kazi nzuri ya kusambaza umeme.

Alisema kwamba kazi hiyo wamekuwa wakifanya kwa kushirikiana na wenzao wabia wa maendeleo wamekuwa msaada mkubwa wakisapoti huo mpango na wametoa fedha nyingi kuhakikisha rea wanasambaza umeme maeneo mengi.

Alisema kwamba sio umeme tu bali hivi karibu kwa kushirikiana n area wamekuwa wakigawa majiko ya nishati safi ya kupikia na wanajua Rais Dkt Samia Suluhu amekuwa kinara wa mpango huo kuhakikisha kwamba Tanzania ifikapo mwaka 2034 watanzania asililia 80 wanakuwa na matumizi ya nishati safi kwa hiyo.

Alisema wanawashukuru wenzao kwa kusapoti jitihada za Rais hivyo sisi kama Serikali tutaendeleza mashirikiano nao kwenye miradi mengine jadidifu ikiwemo joto ardhi kwenye mradi huo na ni miradni inayolenga kupunguza hewa ya ukaa ifikapo mwaka 2034.

Aidha Dkt Mataragio alisema kwa sasa kuna maendeleo makubwa sana ya uhakika wa umeme hapa nchini kwani hata hivi karibuni Naibu Waziri Mkuu hivi karibu Naibu Waziri Mkuu alizindua mtambo wa kuzalisha umeme Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNNH) na sasa hawana mgawo kutokana na uwepo wa uzalishaji wa umeme wa kutosha.

“Kuna matatizo kwenye gridi ambayo Tanesco na Wizara ya nishati tunahakikisha yanatatuliwa tunaendelea kuboresha muindombinu ya kusambaza umeme na kuongeza uzalishaji wa mashine za JNHP zipo 9 moja imekamilika na inazalisha umeme na nyengine imefikia asilimia 99 muda sio mrefu itazinduliwa na itakapokamilika watazindua na wanategemea kutakuwa na umeme wa kutosha “Alisema Dkt Mataragio.

Hata hivyo alisema kwa sasa wana vyanzo vya gesi vinazalisha gesi kama nchi wana umeme wa kutosha maana wana gesi na maji na wanaangalia nishanti nyengine.

Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka watanzania kuchangamkia fursa ya uwepo wa nishati ya umeme kwenye maeneo yao ili kuweza kujikwamua kiuchumi hususani maeneo ye vijijini kutokana na kwamba wakiitumia vizuri inaweza kuwa na manufaa kwao ambayo yatawezesha kuwaongeza kipato huku akiwahimiza wananchi maeneo umeme ulipopita watumie fursa ya kujiunganisha kwenye majumba yao.

Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Batilda Burian alimpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa jinsi alivyoendelea kuhakikisha sekta zote zinakuwa na maendeleo makubwa hususani nishati kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Tanzania nzima imepata umeme na Tanga kwenye vijiji 772 vyote vimepata umepata umeme kasoro 30 na kazi inayoendelea ni kupeleka kwenye vitongoji na wana asilimia 80 imekwenda kwenye vitongoji.

Alisema kupitia kikao hicho cha Wakala huo na wadau wa maendeleo wa nishati kupitia bajeti na kupata fedha za kuongeza ili kuweza kukamilisha vitongoji vilivyosalia kutokana na umuhimu wa umeme katika kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo kwa wananchi kwenye maeneo mbalimbali.

“Umeme ukipatikana unasaidia kuchochea maendeleo na uchumi unakuwa lakini hata vituo vya afya vitafanya kazi,shuleni watoto watasoma tunawashukuru REA wamekuwa wakipeleka Umeme na kuunganisha na mlipokuja Tanga mmeweza kutembelea kituo cha Afya Pangani na mmetoa majiko ya gesi na banifu kwa shule ili kuhakikisha Sera na azma ya Rais Dkt Samia Suluhu ifikapo mwaka 2030 nishati hiyo inatumika tunawashukuru wadau wetu Benki ya Dunia,Benki ya Afrika na wadau wengine wa maendeleo walioshiriki kwenye mpango huu”Alisema

Naye kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassani Saidy alisema hicho ni kikao cha kwanza cha kuandaa mpango kazi na bajeti kwa mwaka ujao wa fedha na serikali imekuwa ikifanya kazi na wadau mbalimbali wa maendeleo kwenye sekta hasa upande wa nishati ya Umeme Vijijini.

“Tunawashukuru wadau tunaoshirikiana nao wakiwemo Benki ya Dunia,Benki ya Afrika,Umoja wa Ulaya,Norway ,Swedeni na MG ya Ufarasa hawa wanachangia kwenye gharama za utekelezaji wa miradi yetu kwa hiyo wananchi wanapoona miradi inaendelea wajue fedha nyingi zinatoka serikali na wadau wanawashirikisha ili kuwaongezea imani yao kuweza kutoa ushirikiano kwemye miradi yao”Alisema Mhandisi Hassani

Mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post