MAAFISA UGANI 1000 KUTOKA MIKOA 7 WAPATA VISANDUKU VYA UGANI

 

Kupitia Bajeti ya kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, Wizara ya Kilimo imefanikisha  ununuzi na usambazaji wa visanduku vya ugani 1000 kwa maafisa ugani Kilimo 1000 katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma, Rukwa na Katavi, sawa na asilimia 25 ya lengo. 

Kwa upande mwingine, tayari magari 46 na Pikipiki 550 kwaajili ya Maafisa ugani ngazi ya mkoa yamelipiwa na wakala wa manunuzi wa Serikali anakamilisha taratibu za manunuzi.

Kuendelea kuimarika kwa huduma za ugani nchini kumewawezesha wakulima kufanya kilimo chenye tija, kuongeza uzalishaji wa mazao na kupunguza hasara ya mavuno hafifu kutokana na kufanya kilimo bila kuwa na taarifa sahihi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post