RC MACHA AZIFARIJI FAMILIA ZILIZOPOTEZA WATOTO KWA KUANGUKIWA NA NYUMBA MVUA IKINYESHA

 Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,ametoa pole kwa Familia ya Mzee Ngassa Mataaluma mkazi wa Kijiji cha Mishepo wilayani Shinyanga, ambayo ilipoteza watoto watatu baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua ambazo zinaendelea kunyesha hapa nchini,pamoja na Familia tatu za Ushetu ambazo nazo zimepoteza watoto.

Amefanya ziara hiyo ya kutoa mkono wa pole leo Aprili 27,2024 alipotembelea Familia hiyo akiwa ameambatana na Kamati yake ya ulinzi na usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoa na Wilaya.

Akizungumza na wananchi pamoja na Familia ya Mzee Ngassa,ametoa pole kwao kutokana na kupoteza watoto wao watatu,huku akitoa wito kwa wananchi kwamba kwa wale ambao wanaishi kwenye nyumba au maeneo hatarishi, ni vyema wakahama kwenye makazi yao hasa katika kipindi hiki cha Mvua nyingi ili kunusuru maisha yao.

Amesema Serikali ipo pamoja na Familia hiyo, na kutoa maagizo kwa viongozi wa Serikali ngazi ya Kata kwamba wakae pamoja na wananchi ili kuona namna ya kuisaidia familia hiyo kuijengea nyumba ambapo Mkoa utawashika Mkono ili warudi kuishi kama hapo awali.
“Poleni sana Familia ya Mzee Ngassa Mataaluma pamoja na wananchi wa Kijiji cha Mishepo, kwa kuondokewa na watoto wenu watatu kwa kupoteza maisha sababu ya kuangukiwa na nyumba, na sisi Serikali tukakuwa nanyi bega kwa bega pamoja na kuhakikisha mnapata nyumba nyingine tena imara,”amesema Macha.

Amewapongeza pia majirani ambao wameichukua Familia ya Mzee Ngassa na kuwatunza kwa muda kutokana na kukosa makazi baada ya nyumba yao kuanguka, na kutoa wito kwa wananchi kwamba wapendane pamoja na kusaidiana kuishi na wenzao ambao nyumba zao zipo katika maeneo hatarishi.
Aidha,Mkuu wa Mkoa ametoa Sare za Shule kwa Mtoto Matiza Ngassa (8) ambaye alinusurika kifo baada ya nyumba yao kuanguka, pamoja na kuonyesha ujasiri wa kumuokoa Mama yake na kutoa taarifa kwa majirani.

Katika hatua nyingine RC Macha, ametoa pole katika Familia nyingine Tatu za Halmashauri ya Ushetu, ambao zilipata Maafa kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini na kusababisha vifo vya watoto.
Watoto watatu waliopoteza maisha katika Familia ya bwana Ngassa Mataaluma Kijiji cha Mishepo, ni Nkamba Ngassa (13),Gigwa Ngassa (8) na Salumu Ngassa(6).

Watoto waliopoteza maisha huko Ushetu ni Paulo Matisho (4),Emmanuel Charles (3) na Nicholaus Focus (3) ambao wote walipoteza maisha Aprili 26 mwaka huu, kwa kuangukiwa na nyumba baada ya mvua kubwa kunyesha.
Naye Mzee Ngassa Mataaluma, amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kumtembea katika Familia yake na kumpatia Mkono wa pole, huku akiishuru Serikali kwa kuwa naye bega kwa bega tangu siku ya tukio hadi sasa wapo pamoja naye.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akimpatia Mkono wa pole Kashinje Nchembi Mama ambaye amepoteza watoto wake watatu baada ya kuanguliwa na nyumba katika Familia ya Ngassa Mataaluma katika Kijiji cha Mishepo wilayani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akimpatia Mkono wa pole Mtoto Matiza Ngassa ambaye alinusurika kifo na wenzake watatu kufariki baada ya kuanguliwa na nyumba.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mishepo wilayani Shinyanga alipofika kutoa pole katika Familia ya Ngassa Mataaluma ambaye amepoteza watoto wake watatu kwa kuangukiwa na nyumba.
Wananchi wa Kijiji cha Mishepo wilayani Shinyanga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Annamringi Macha alipofika kutoa pole katika Familia ya Ngassa Mtaaluma ambaye amepoteza watoto wake watatu kwa kuangukiwa na nyumba.

Muonekano wa nyumba ya Familia ya bwana Ngassa Mataaluma ambayo imeanguka na kupoteza watoto wake watatu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post