WASABATO WAHITIMISHA SEMINA MAALUMU YA MAFUNDISHO YA AFYA,BIASHARA,KAYA NA FAMILIA

 Na Marco Maduhu,SHINYANGA
KANISA la Waadventista Wasabato ukanda wa dhahabu Nyanza Gold Belt Field (NGBF),wamehitimisha Semina Maalumu ya Mafundisho ya Afya, Biashara, Kaya na Familia iliyowakutanisha watu mbalimbali mkoani Shinyanga.

Mafundisho hayo yalianza kutolewa Aprili 21 mwaka huu na kuhitimishwa leo, ambayo yalifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Akizungumza wakati wa kufunga Mafundisho hayo Askofu wa Jimbo ukanda wa dhahabu (NGBF) Kanisa la Waadventista Wasabato Enock Sando, amesema Kanisa linawajibu wa katika jamii,kugusa jamii na kuiongezea thamani na ndiyo maana limeendesha Semina hiyo.

“Kanisa la Wasabato tusijifungie ndani bali tutoke na kuongeza thamani jamii kupitia mafundisho mbalimbali, na katika Semina hii ambayo tumeindesha itakuwa imewabadilisha watu kwa namna moja ama nyingine, na hawezi kutoka hivi hivi bali kunakitu ambacho wamekipata,”amesema Askofu Sando.
Aidha, katika Semina hiyo baada ya Watalaamu wa Afya ambao wametoa mafundisho alikuwapo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk.Luzila John,Asnathi,Maufi na Madanka, ambapo Somo la Biashara lilitolewa na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Shinyanga (TCCIA) Jonathani Manyama, huku Somo la Kaya na Familia likitolewa na Mchungaji Mstaafu Wilbert Nfumbusa.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Askofu wa Jimbo ukanda wa dhahabu (NGBF) Kanisa la Waadventista Wasabato Enock Sando akizungumza wakati wa kuhitimisha Semina hiyo.
Askofu wa Jimbo ukanda wa dhahabu (NGBF) Kanisa la Waadventista Wasabato Enock Sando akizungumza wakati wa kuhitimisha Semina hiyo.
Mchungaji Mstaafu Wilbert Nfumbusa akitoa Somo la Kaya na Familia kwenye uhitimishaji wa Semina hiyo.
Kamati ya Maandalizi ya Semina hiyo ikimuagua Mchungaji Mstaafu Wilbert Nfumbusa na kumpatia zawadi ya pesa.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk. John Luzila akiwa kwenye Semina hiyo.
Washiriki wakiwa kwenye Semina kabla ya kuhitimishwa.
Kamati ya Maandalizi ya Semina hiyo.
Semina ikiendelea kabla ya kuhitimishwa.
Washiriki wakiendelea na Semina.
Washiriki wakiendelea na Semina.
Washiriki wakiendelea na Semina.
Washiriki wakiendelea na Semina.
Washiriki wakiendelea na Semina.
Washiriki wakiendelea na Semina.
Washiriki wakiendelea na Semina.
Washiriki wakiendelea na Semina.
Washiriki wakiendelea na Semina.
Kwaya ya Maranatha kutoka Kanisa la Wasabato Lubaga ikiimba kwenye Semina hiyo.
Kwaya ya Maranatha kutoka Kanisa la Wasabato Lubaga ikiimba kwenye Semina hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post