AMUUA MWENZAKE MZOZO WA SIMU


Kijana aliyeuawa

Kijana Shaban Athuman Mgosi (39) mkazi wa Majengo Mapya mjini Moshi ameuawa leo Aprili 24, 2024 majira ya saa 12:20 asubuhi baada ya ugomvi baina yake na rafiki yake kuhusu masuala ya simu.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema siku za hivi karibuni walikuwa wakivutana na rafiki yake kuhusu simu ambapo asubuhi ya leo alimwamsha kama anataka kuzungumza naye ndipo alipomkata na kitu chenye ncha kali maeneo ya shingo na kijana huyo kufariki papo hapo.

Mtuhumiwa wa mauaji hayo anayefahamika kwa jina la Rajabu amekimbia kusikojulikana ambapo katika chumba cha mtuhumiwa ilionekana simu ikiwa imetapakaa damu.

Mwenyekiti wa Mtaa huo Bi. Kimambo amethibitisha kuwapigia simu Polisi ambao walifika mara moja eneo la tukio na kuubeba mwili wa marehemu kwa hatua zaidi za uchunguzi.

CHANZO -  EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post