AMUUA MWENZAKE KWA KISU WAKICHEZA MUZIKI BAAMkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam, Kadi Msela, ameuawa kwa madai ya kuchomwa kisu na rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Amir, wakati wakicheza muziki baa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amethibitisha tukio hilo lililotokea Aprili 20, mwaka huu.

Akizungumza na Nipashe Digital, Muliro amesema: “Ni kweli kuna tukio hilo la kijana Kadi kufariki dunia kwa madai ya kuchomwa kisu na rafiki yake Amir. Taarifa za awali zinaeleza kwamba wawili hao walikuwa marafiki na walitofautiana.”

Kamanda Muliro amesema kwa mujibu wa mashuhuda kijana huyo alichomwa kisu sehemu ya shingoni wakati wakicheza muziki katika baa moja iliyokuwa ikizinduliwa eneo la Tegeta.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post