HAKIELIMU WAJA NA MKAKATI MPYA KUSAIDIA WASICHANA WALIOKATIZA MASOMO YAO

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.

*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DODOMA

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia watatumia matokeo ya tafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito katika kuhakikisha wanaboresha Malezi na Makuzi ya Watoto pamoja na Elimu ya Wasichana waliorejea shuleni baada ya kujifungua.

Hayo yamesemwa Aprili 29, 2024 Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula wakati akizindua Ripoti hizo mbili.

Alisema zipo taarifa ambazo kama Wizara wanazisikia kuhusu Utekelezaji wa mpango huo wa kurejea shuleni kwa wasichana waliokatiza masomo kwa ujauzito ambazo zinaonesha mafanikio na changamoto

“Utafiti huu utatusaidia sana katika hukakiki taarifa tulizonazo na kufuatilia jinsi wasichana, jamii, walimu na wadau wengine wanavyopokea na kutumia fursa hii muhimu” alisema Dkt. Rwezimula.

Aidha Dkt. Rwezimula alisema matokeo ya utafiti yataiwezesha Serikali na wadau wakuu katika elimu kutatua changamoto zilizopo katika utekelezaji wa mpango huo Jumuishi.

“Hii itawezesha watoto wote Tanzania kuwa kwenye mwelekeo sahihi wa kufikia ukuaji timilifu kwa kuwajengea misingi ya kuwa watu mahiri wenye ujuzi na uwezo wa kuchangia maendeleo ya taifa pindi wanapokua watu wazima” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt. John Kalage alisema kuwa HakiElimu imefanya tafiti hizo kama sehemu ya jukumu lake la kuzalisha taarifa zenye ushahidi kwa ajili ya utekelezaji wa sera, hususani katika eneo la malezi na makuzi ya mtoto, ambalo ni mojawapo ya vipaumbele vya shirika katika mpango Mkakati wao wa miaka mitano (2022-2026).

Alisema tafiti hizo mbili ni tofauti, kwa pamoja zinaunganishwa na dhana ya ustawi wa watoto kwa ujumla wao kuanzia umri wa kuzaliwa hadi miaka nane.

“Kama tunavyojua, suala la kuwarejesha shuleni wasichana wanaopata ujauzito (ambalo tumekuwa tukilipigania kwa muda mrefu) sio tu linahusu kutoa fursa kwa wasichana wanaopata ujauzito wakiwa shuleni, bali pia linahusu ustawi wa watoto wanaozaliwa” alisema Dkt. Kalage.

Pamoja na hayo alisema utambuzi wa mazingira ya ustawi wa malezi na makuzi ya mtoto utasaidia namna jamii, serikali na wadau wengine, sio tu kuja na mkakati mzuri wa kumsaidia mtoto anayezaliwa bali pia mama yake ambaye ki sheria bado pia ni mtoto na mwanafunzi.

“Kama mtakavyosikia kutoka kwa watafiti viongozi, eneo la malezi na makuzi ya mtoto sio tu ni nyeti bali pia lina changamoto nyingi, ambazo ufumbuzi wake unahitaji ushiriki wa kila mdau katika jamii” alieleza Dkt. Kalage.

Hata hivyo Dkt. Kalage aliipongeza Serikali na taasisi zake kama vile COSTECH, NIMRI, Vyuo Vikuu vya DSM na UDOM, TAMISEMI na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zimeruhusu tafiti hizo kufanyika na kuwapatia kila msaada waliohitaji katika kuwezesha tafiti hizo.

Alisema Ushirikiano huo si tu unawapa fursa ya kuchangia katika uzalishaji wa taarifa za utafiti, lakini pia kutoa mchango katika uboreshaji wa huduma za malezi na makuzi ya mtoto na upatikanaji wa elimu nichini Tanzania.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu wakati akizindua ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage wakati akizindua ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi HakiElimu Richard Mabala (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi Msaidizi idara ya Maendeleo ya Watoto Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mathias Haule pamoja na Mkuu wa Miradi HakiElimu, Godfrey Boniventura wakionesha ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito mara baada ya kuzindua Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi HakiElimu Richard Mabala (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi Msaidizi idara ya Maendeleo ya Watoto Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mathias Haule pamoja na Mkuu wa Miradi HakiElimu, Godfrey Boniventura wakionesha ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito mara baada ya kuzindua Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi HakiElimu, Richard Mabala akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage, Mwenyekiti wa Bodi HakiElimu Richard Mabala, Mkurugenzi Msaidizi idara ya Maendeleo ya Watoto Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mathias Haule pamoja na Mkuu wa Miradi HakiElimu, Godfrey Boniventura wakipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Elimu nchini wakati wa uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage, Mwenyekiti wa Bodi HakiElimu Richard Mabala, Mkurugenzi Msaidizi idara ya Maendeleo ya Watoto Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mathias Haule pamoja na Mkuu wa Miradi HakiElimu, Godfrey Boniventura wakipata picha ya pamoja na Watumishi wa HakiElimu wakati wa uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage, Mwenyekiti wa Bodi HakiElimu Richard Mabala, Mkurugenzi Msaidizi idara ya Maendeleo ya Watoto Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mathias Haule pamoja na Mkuu wa Miradi HakiElimu, Godfrey Boniventura wakipata picha ya pamoja na viongozi na wawakilishi wa Mashirika ya Maendeleo yasiyo ya Kiserikali wakati wa uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya HakiElimu Richard Mabala wakati wa uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Wadau mbalimbali wa elimu nchini wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Mtafiti Mkuu na Mhadhiri Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Dkt. Joyce Mbepera akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada katika uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.
Mshauri Mwelekezi na Mtafiti Mwenza-HakiElimu akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada katika uzinduzi wa ripoti mbili za Utafiti Kuhusu Hali ya Jumla ya Elimu na Makuzi ya Mtoto na Kurejeshwa Shuleni kwa Wasichana Waliokatiza masomo kwasababu ya Ujauzito uliofanyika Aprili 29, 2024 katika hoteli ya New Dodoma iliyopo Jijini Dodoma.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post